25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SEBASTIAN NKOMA NATENGEZA TWIGA STARS MPYA

Na MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM


TIMU ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite Queens’ inajiandaa na mchezo wa awali kutafuta nafasi ya kufuzu fainali za dunia kwa wanawake wa umri huo, dhidi ya Nigeria.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza, utachezwa Septemba 17 mwaka huu, jijini Lagos, Nigeria, kabla ya marudio yake kufanyika hapa nchini wiki mbili baadaye.

Mshindi wa jumla wa mchezo huo, atafuzu kucheza mechi mbili na Morocco, ambapo mshindi atakata tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki fainali za dunia zitakazofanyika Desemba mwaka huu, nchini Ufaransa.

Timu hiyo imeweka kambi kwa zaidi ya wiki mbili katika hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, unaomilikiwa na shirikisho hilo.

SPOTIKIKI ilifanya mahojiano maalumu na kocha mkuu wa Tanzanite Queens, Sebastian Nkoma, ambaye anaamini timu hiyo itafanya vema, licha ya kukosa mechi za majaribio.

MTANZANIA: Unazungumziaje maandalizi ya timu?

Nkoma: Maandalizi tulianza wiki mbili zilizopita, lakini kabla ya hapo niliomba nipate kambi ya kila mwezi japo ilishindikana kwa sababu wachezaji wanaounda timu hii kuwa mashuleni.

MTANZANIA: Kikosi hicho kiliundwa vipi?

NKOMA: Kikosi kamili kina wachezaji 25, lakini nilionao kambi hadi sasa ni wachezaji 21, wanne tumeshindwa kuwapata kutokana na kubwa na ratiba za mitihani katika shule wanazosoma.

Nkoma: Wachezaji wote ni wanafunzi, wengi tumewapata mashuleni na wengine katika mashindano mbalimbali, tuliyofanya kwa ajili ya kuchagua wachezaji wa kuunda timu hii.

MTANZANIA: Kikosi kina muda gani tangu kilipoundwa?

Nkoma: Kwa kweli kikosi hichi  ni kipya, hakina muda mrefu nilianzisha timu hii ili kutengeneza mbadala sahihi wa wachezaji wa timu ya Twiga Stars.

Nkoma: Twiga Stars kwa kipindi kirefu ilikuwa na wachezaji 30, hata wakati wa kuitwa timu hiyo kambini walikuwa wanajijua kabisa, hivyo niliamua kutengeneza vijana wengine ambao watasaidia kuwepo kwa wigo mpana wakati wa uchaguzi wa wachezaji wa timu ya Taifa. Na nilifanya hivyo kutokana na kukosekana kwa mashindano ya timu za wanawake.

MTANZANIA: Umejipangaje kuhakikisha program yako ya kupata mbadala wa Twiga Stars  yanatimia?

Nkoma: Programu ikipata sapoti itakua tu, hivyo nawaomba  wadau wa soka wanisaidie, kwani timu za wanawake zimekuwa zikifanya vizuri sana kwenye michuano ya kimataifa tofauti na wanaume.

Nkoma: Endapo nitaendelea kupata sapoti, nimepanga kuanzisha program ya timu ya umri wa chini wa miaka 17, hii itasaidia mgawanyo mzuri wa timu hizi na imani yangu kwa kiasi kikubwa  kikosi cha Twiga Stars kitaimarika.

MTANZANIA:Changamoto unazokutana nazo kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Nigeria?

Nkoma: Hadi sasa tumefanikiwa kucheza mchezo mmoja pekee wa kirafiki dhidi ya Twiga Stars, matokeo yalikuwa sare bao 1-1.

Nkoma: Tuliomba kupata michezo miwili ya kirafiki na nilipendekeza timu za Kenya na Uganda, hadi sasa hakuna kilichofanikiwa na TFF wamesema wanaendelea kufuatilia.

MTANZANIA: Kutokana na uchanga wa kikosi, huoni kuwa itakuwa sababu ya kupata matokeo mabovu Lagos?

Nkoma: Ni kweli kikosi chetu ni kichanga, kwani mchezo huu utakuwa wa kwanza wa kimashindano, lakini kupitia mazoezi ambayo naendelea kuyatoa kwa wachezaji wangu natumaini hawataniangusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles