SCOTT   SASA MAMBO NI  MOTO KWA  SOFIA

0
701

LOS ANGELES, MAREKANI


NYOTA wa tamthilia ya ‘Keep up with Kardashian’, Scott Disick na Sofia Richie, wameonekana tena  mtaani safari hii wakioneshana mapenzi moto moto.

Scott mwenye umri wa miaka 34 Jumamosi iliyopita alikutwa na  mrembo, Sofia (19),  katika fukwe ya Malibu  mjini Los Angeles, Marekani  wakijiachia. Mara ya mwisho wapenzi hao kukutwa pamoja ilikuwa wiki mbili zilizopita.

Scott na Sofia wamekuwa pamoja miezi kadhaa iliyopita, baada ya  mwaka 2015 kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu Kourtney Kardashian, ambaye  walibahatika kupata watoto watatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here