29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Scorpion kufunguliwa shitaka jipya

scorpionMAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala mchana huu inatarajia kumfungulia shitaka jipya Salum Henjewele maarufu Scorpion baada ya shitaka la awali la unyang’anyi wa kutumia silaha kufutwa.

Awali Mahakama hiyo ililazimika kufuta shitaka hilo kufuatia maombi yaliyowasilishwa na Mwendesha Mashitaka, Munde Kalombola ambaye aliiomba mahakama hiyo kufutwa kwa shauri hilo mbele ya Hakimu Mkazi Adelf Sachore ambaye aliridhia maombi hayo baada ya upande wa mashtaka kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo.

“Kutokana na maombi yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka, Mahakama imeliondoa shitaka hili kama ilivyoombwa kupitia kifungu cha 91 kifungu kidogo cha 1,” alisema Hakimu Sachore.

Kifungu hicho cha 91(1) kinampa mamlaka DPP kuliondoa shitaka hilo, Scorpion anatarajiwa kufunguliwa mashitaka mapya mchana huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles