24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘Scorpion’ afanya vituko mahakamani

Mtuhumiwa wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Henjewele, maarufu kama ‘Scorpion’ akiwa chini ya ulinzi wakati akitoka katika chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam jana. Picha ndogo ni mtuhumiwa huyo wakati akiingia mahakamani.
Mtuhumiwa wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Henjewele, maarufu kama ‘Scorpion’ akiwa chini ya ulinzi wakati akitoka katika chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam jana. Picha ndogo ni mtuhumiwa huyo wakati akiingia mahakamani.

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

SALUM Henjewele (34) maarufu kama ‘Scorpion’  mkazi wa Yombo Machimbo anayetuhumiwa kumchoma kisu na kumtoa macho, Saidi Mrisho jana aliwashangaza watu kwa kufanya vituko mahakamani.

Katika hali ya kushangaza, mtuhumiwa huyo alibadilisha mavazi yake akiwa mahakamani, ili asijulikane mbele ya umati wa watu waliokuwa wamefurika mahakamani hapo.

‘Scopion’ ambaye ni mwalimu wa mashwati (karate) anadaiwa alifanya tukio hilo Septemba 6 mwaka huu eneo la Buguruni Sheli Jijini Dar es Salaam.

Akiwa anatoka mahakamani ‘Scorpion’ alionekana amevaa nguo tofauti na zile alizokuwa amevaa asubuhi wakati kesi yake ikitajwa.

Awali mtuhumiwa huyo alivaa fulana nyekundu na suruali ya jeans ya bluu, tofauti na mchana ambapo alionekana amevalia baragashia kichwani na shati la mikono mirefu lenye rangi ya kijivu.

Mavazi hayo yaliwachanganya baadhi ya watu waliokuwa na shauku ya kutaka kumwona akipanda gari la magereza. Hata hivyo waandishi wa habari na wapiga picha walishtukia ‘janja’ hiyo na kumtambua kwa haraka.

Awali, Scorpion alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Adelf Sachore kwa kuongozwa na  Wakili wa Serikali, Munde Kalombola kwa ajili ya kutajwa kwa shauri la unyang’anyi wa kutumia silaha na kumsababishia upofu wa kudumu, Said Mrisho kwa kumtoboa macho.

Hata hivyo shauri hilo liliahirishwa hadi  Oktoba 19 mwaka huu litakapotajwa tena.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya kesi hiyo namba 276 ya mwaka 2016 ilitajwa kwa mara ya kwanza Septemba 28, mwaka huu.

Hata hivyo mshtakiwa huyo jana alionekana mtu asiye na wasi wasi, huku akitabasamu muda wote.

Katika hati hiyo ya mashtaka, ilidaiwa kuwa, Septemba 6 mwaka huu saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Sheli Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, aliiba cheni ya Silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000 na black bendi ya mkononi pamoja na fedha taslimu Sh 330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000 mali ya Said Mrisho.

Hati hiyo ilielezwa kuwa kabla na baada ya kutekeleza tukio hilo, mtuhumiwa huyo alimchoma, Mrisho sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo machoni, tumboni na mabegani ili kurahisisha kupata mali hizo.

Mama mzazi wa Mrisho

Nje ya mahakama hiyo, mama mzazi wa Mrisho aitwaye Halima Jissu pamoja na ndugu na jamaa zake walikuwa wakilia muda wote huku wakisema wanamwachia Mungu kwa kilichotokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles