28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Scholes awaaminisha United kwa Barcelona

MANCHESTER, ENGLAND

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes, anawaaminisha wachezaji wa timu hiyo kuwa, wanaweza kuishangaza dunia katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Barcelona kutokana na kiwango cha wapinzani hao kwa sasa.


Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali unatarajiwa kupigwa kesho kwenye uwanja wa Camp Nou, baada ya mchezo wa awali wiki iliyopita ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford na Man United kukubali kichapo cha bao 1-0.


Scholes anaamini kuwa Barcelona msimu huu hawana ubora mkubwa kulinganisha na wababe wa soka nchini Ufaransa, PSG. Manchester United wamefanikiwa kuingia hatua hiyo ya robo fainali baada ya kuwafunga PSG mabao 3-1, huku PSG wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani baada ya mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Old Trafford kumalizika kwa United kukubali kichapo cha mabao 2-0.


Kama walivyofanya Man United kwenye Uwanja wa PSG, basi Scholes anaamini kesho wanaweza kufanya hivyo kwenye Uwanja wa Camp Nou.


“Sidhani kama Barcelona wana ubora ule ambao tumeuona kwa miaka kadhaa iliyopita. Manchester United ilikwenda nyumbani kwa PSG na wakafanya kazi kubwa sana na kufanikiwa kuibuka na ushindi, hivyo ninaamini kwa sasa wao ni bora kuliko Barcelona,” alisema mchezaji huyo wa zamani, ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa michezo.


Manchester United wanahitaji ushindi wa aina yoyote kuweza kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali, wakati huo Barcelona wakihitaji sare yoyote au ushindi, hivyo mchezo huo unaonekana utakuwa mgumu, hasa kwa Manchester United kuweza kutamba kwenye uwanja huo wa ugenini.


Barcelona watashusha kikosi chao chote ili kuhakikisha wanafanikiwa kusonga , kwa kuwa sasa hawana wasiwasi na michuano ya Ligi Kuu Hispania kutokana na pointi walizonazo, ambazo zinawapa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu, hivyo akili yao kwa sasa ni kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles