29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Savage adondosha ‘Your Waist’ X King Perry, Psycho YP

Na Joseph Shaluwa, Mtanzania Digital

MSANII wa muziki wa Rap kutoka Nigeria, Savage a.k.a Savage tha Beast amerejea tena na wimbo wake mpya ‘Your Waist’ akiwa amegonga kolabo na King Perryy na PsychoYP.

Wimbo huo wa Hip-Hop na Rap una vionjo vya aina yake, huku mapigo ya Afro-Dancehall yaliyochagizwa na King Perryy ukizidisha utamu wa ngoma hiyo ambayo tayari imeshakuwa gumzo kwenye mitandao.

Video ya muziki ya wimbo huo inamuonesha Savage akiigiza kama mkurugenzi akiwa pamoja na Moustacheboy.

Wimbo wa kwanza wa Savage “Confident” akimshirikisha Buju uliunda utambulisho mzuri katika tasnia ya muziki, ikifuatiwa na albamu yake ya kwanza ya mwaka 2021 ‘Utopia’ iliyofungua njia yake na kuruhusu ushirikiano na mastaa mbalimbali wakiwemo Kojo Funds, Kida Kudz, Alpha P, Emtee na staa kutoka Kenya, Khaligraph Jones.

Savage ambaye ana umri wa miaka 27 sasa, ameanzisha timu ya wabunifu inayoitwa ‘Savage Space’ inayohusika katika mwelekeo wa ubunifu, mavazi – Savage Space Couture.

Awali, Savage alianza kufanya muziki akiwa na umri wa miaka 16 chini ya  bendi ya watu sita iliyoitwa “Team Nawty” iliyojumuisha marafiki kutokana na mapenzi yao kwa muziki.

Akiwa anatoka Uzere, Jimbo la Delta, Savage ni Mnigeria mwenye fahari anayewakilisha nchi yake ya asili na kuwatia moyo vijana wote kutoka Nigeria pamoja na Waafrika wenzake kupitia sanaa yake inayomnufaisha vilivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles