JEREMIA ERNEST
Tamasha la Sauti za Busara 2020, linatarajiwa kufanyika Mji Mkongwe, Unguja Februari 13 hadi 16, ambapo waandaaji wameamua kutilia mkazo suala la unayanyasaji wa kijinsia.
Ikiwa huu ni msimu wa 17 toka kuanzishwa kwa Sauti za busara nchini imekua na utamaduni wa kukutanisha wasanii wa muziki wa asili kutoka sehemu mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa tamasha hilo, Yussuph Mahmud amesema tamasha hilo lina faida kubwa hapa nchini pamoja na kwa wasaniii wanaopata nafasi ya kushiriki.
“Tamasha hili limekua likitoa ajira, linakuza uchumi pia linatangaza utalii wa nchi kwa kuwa watu wengi wanakuja kushiriki tamasha hili na wasanii ambao wanashiriki wanapata baada ya hapo hupata mualiko nchi jirani,” amesema Yussuph.
Wasanii ambao wamepata dili la kutumbiza katika tamasha hilo mwaka huu ni Siti & the Band (Zanzibar) na This Diarrana Mamy Kanouté kutoka Afrika Magharibi.