25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Saudia yakiri kuhusika kifo cha Khashoggi

RIYADH, SAUDI ARABIA


UTAWALA wa Kifalme nchini Saudi Arabia umekiri kuwa mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi aliuawa katika ubalozi wake mdogo mjini Istanbul nchini Uturuki, baada ya kile ilichokitaja ugomvi.

Maelezo ya utawala huo yameaminika mbele ya Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye amesema licha ya kupokelewa kwa mashaka na wabunge wa Marekani, lakini kuna usahihi wa taarifa za Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Al Jazeera, utawala wa Saudi Arabia umetangaza kuwakamata watu 18 kuhusiana na sakata hilo la Khashoggi na wasaidizi wawili wakuu wa mrithi wa ufalme Mohamed Bin Salman wamefutwa kazi.

Khashoggi, ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Marekani la Washington Post na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Kifalme wa Saudi Arabia, alionekana mara ya mwisho akiwa hai  mnamo Oktoba 2, mwaka huu alipoingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabia kuchukua hati za kumruhusu kufunga ndoa.

Kukiri huko kwa Saudi Arabia kuwa mwandishi huyo ameuawa baada ya kukanusha mara kadhaa kunakuja baada ya Marekani kutishia kuiwekea nchi hiyo vikwazo.

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Saudi Arabia, Sheikh Saud al Mojeb, amesema Khashoggi aliuawa baada ya ugomvi uliosababisha mapigano kati yake na watu waliokutana naye ubalozini.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,407FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles