27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Saudi Arabia yawakamata wanawafalme watatu

RIYADH, SAUDI ARABIA

NDUGU watatu wa familia ya kifalme ya Saudia Arabia akiwemo nduguye mwanamfalme wa Saudia, Mohammed bin Salman wamekamatwa kwa sababu zisizojulikana.

Kukamatwa kwao kuonaonesha jinsi mwanamfalme Mohammed bin Salman anavyojaribu kuimarisha uwezo wake wa kutawala.

Mwaka 2017, wanawafalme kadhaa, mawaziri na wafanyabiashara walikamatwa katika hoteli ya Ritz -Carlton mjini Riyadh baada ya mwanamfalme huyo kuamrisha kukamatwa kwao.

Mohammed Bin Salman, anayepewa sifa ya  utata ndiye  kiongozi anayetajwa kuwa mkuu wa ufalme huo baada ya kuchukua utawala kutoka kwa baba yake mwaka 2016.

Kukamatwa kwao kwa mara ya kwanza kulifichuliwa na gazeti la Wall Street ambalo linasema kitendo hicho kilifanyika mapema siku ya Ijumaa.

Ndugu hao watatu waliokamatwa ni ndugu yake mdogo mwanamfalme huyo, Ahmed bin Abdulaziz, aliyekuwa mwanamfalme Mohammed bin Nayef, na binamu yao mwanamfalme Nawaf bin Nayef.

Mohammed bin Nayef alikuwa waziri wa mambo ya ndani hadi alipoondolewa katika wadhfa wake na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani na Mohammed bin Salman mwaka 2017.

Katika jukumu lake la awali alionekana kama mtu wa karibu na anayeaminika na maofisa wa ujasusi wa Marekani.

Prince Ahmed bin Abdulaziz, mwenye umri wa 78, ndiye nduguye mwanamfalme huyo aliyesalia.

Mwaka 2018 alitoa matamshi yalioonekana yakimkosoa Mohammed bin Salman dhidi ya waandamanaji mjini London lakini baadaye akasema kwamba alinukuliwa visivyo.

Wote wawili walionekana kuwa wapinzani wa mwanamfalme huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye anaongoza katika wale watakaochukua ufalme wa taifa hilo.

Walinzi waliwasili katika nyumba za wanawafalme hao wakiwa wamevalia barakoi na kuvaa mavazi meusi na kupekua mali , lilisema jarida hilo la Wall Street.

Mwandishi wa masuala ya usalama- Frank Gardner katika uchambuzi wake anasema hii ni hatua muhimu ya mwanamfalme Mohammed bin Salman ili kushilkilia mamlaka .

Mwanamfalme Ahmed bin Abdelaziz ni mmoja wa watoto waliosalia wa mwanzilishi wa taifa hilo mfalme Abdelaziz, na mtu anayeheshimika sana miongoni mwa watu wa familia hiyo ya kifalme.

Mwanamfalme mwingine mkuu ni Mohammed bin Nayef , ambaye pia alikuwa miongoni mwa warithi wa ufalme huo kabla ya kuondolewa kwenye uongozi miaka mitatu iliyopita.

Kabla ya hatua hiyo , alikuwa waziri wa mambo ya ndani nchini humo  na alisifiwa sana kwa kuwashinda wapiganaji wa al- Qaeda waliokuwa Saudia miaka 2000.

Hakuna thibitisho rasmi ama katazo lolote kuhusu taarifa iliyochapishwa katika vyombo vya habari vya Marekani licha ya kwamba masuala ya kifalme nchini Saudia hufanywa kwa siri kubwa.

Mwanamfalme Mohammed bin Salman alipata sifa za kimataifa 2016 wakati alipoahidi msururu wa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika taifa hilo lenye utamaduni wa kihafidhina.

Hatahivyo amepata kashfa kadhaa ikiwemo ile ya mauaji ya mwandishi wa Saudia Jamal Khashoggi katika ubalozi wa Saudia uliopo mjini Istanbul 2018.

Pia amekosolewa kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Yemen ambapo wanajeshi wa serikali wanaoungwa mkono na Saudia pamoja na unyanyasaji wa wanaharakati wanawake licha ya kuondoa vikwazo ikiwemo haki ya kuendesha magari.

Katika siku za hivi karibuni amekuwa akichukua hatua za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa hatari wa virusi vya corona.

Mahujaji wa kigeni wamezuilia kuingia nchini humo ili kushiriki katika ibada ya Umrah ama kuhiji na kuna maswali ya iwapo ibada ya hajj ya kila mwaka itafanyika mwaka huu.

Alhamisi mji mtakatifu wa Kiislamu wa Mecca ulifanyiwa usafi wa kiwango cha juu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,554FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles