SAUDI ARABIA YABADILI MTAZAMO KUHUSU ISRAEL

0
608

RIYADHI, SAUDI ARABIA


MRITHI wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman amesema Israel ina haki ya kuishi kwa amani katika ardhi yao.

Tamko hilo linaloashiria kubadilika kwa mtizamo wa ufalme huo kuhusu Israel na Palestina.

Katika mahojiano yaliyochapishwa na Gazeti la Marekani la The Atlantic, bin Salman amesema Wayahudi wana haki ya kuwa na taifa katika ardhi ya mababu zao, kauli inayoashiria kuimarika kwa uhusiano kati ya Saudi Arabia na Israel.

Nchi hizo mbili hazina uhusiano rasmi wa kidiplomasia lakini uhusiano umeboreka katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Saudi Arabia ambayo ni kitovu cha Uislamu, imekuwa haiitambui Israel na kusisitiza kwa miaka mingi kuwa uhusiano wa kawaida kati yao utarejea iwapo itaondoka kutoka ardhi ya Waarabu.

Ardhi hiyo iliyochukua kwa nguvu katika vita vya mwaka 1967 vya Mashariki ya Kati, maeneo ambayo Wapalestina wanatumaini kujenga taifa lao katika siku za usoni.

Kuongezeka kwa uhasama kati ya Iran na Saudi Arabia kumechochea fununu kuwa maslahi ya pamoja huenda yakaipelekea Saudi Arabia na Israel kushirikiana zaidi dhidi ya Iran inayotizamwa kama kitisho chao kikubwa.

Nchi hizo mbili mbali ya kuichukulia Iran pia zinaichukulia Marekani kama mshirika wao mkuu na zote zinaona tishio kutoka kwa makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali.

Bin Salman yuko katika ziara ya wiki tatu nchini Marekani kutafuta kufikia makubaliano kuhusu uwekezaji na kutafuta uungwaji mkono katika kudhibiti ushawishi wa Iran katika ukanda wa Mashariki ya kati

Amesema anaamini kuwa kila mtu kokote kule ana haki ya kuishi katika taifa lenye amani na anaamini Waisrael na Wapalestina wana haki ya kumiliki ardhi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here