24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Sarri ataka Chelsea kufanya uamuzi mgumu kwa Hazard

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa Chelsea, Maurizio Sarri, ameitaka klabu yake kufanya uamuzi mgumu ili kufunga mjadala wa hatima ya mshambuliaji wa timu hiyo, Eden Hazard.

Hazard (27), ambaye amefikisha mabao 100 baada ya hivi karibuni Chelsea kuifunga Watford mabao 2-1 katika Ligi Kuu England, anatamani kuwa mchezaji mkongwe katika klabu hiyo.

Raia huyo wa Ubelgiji mkataba wake unamalizika Juni mwaka 2020, anahusishwa kuhamia klabu ya Real Madrid.

Lakini wakati Chelsea ikijiandaa kutua dimbani leo dhidi ya Crystal Place katika Uwanja wa Selhurst Park, kocha Sarri alisema klabu hiyo inatakiwa kupata ufumbuzi kuhusu hatima ya mshambuliaji huyo haraka.

Akiulizwa swali kama ana matarajio yoyote ya kumbakisha nyota huyo, Sarri alisema: “Sifahamu lakini huu ni muda wa klabu kufanya uamuzi.”

Oktoba mwaka huu Hazard alisema ni ndoto yake kucheza Real Madrid licha ya siku mbili baadaye kukataa kuwa katika mipango ya kujiunga na klabu hiyo  katika usajili wa dirisha dogo litakalofunguliwa keshokutwa.

Baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Watford FC, Hazard alisema: “Nahitaji kufunga zaidi kwa faida ya timu yangu na baadaye kuwa mchezaji mkongwe kama Frank Lampard, Didier Drogba na John Terry.”

Lakini Sarri alisema: “Sina nguvu katika kuamua hili, mimi ni kocha wala si rais wa klabu au mkuu wa masoko. Nahitaji kuzungumza naye kuhusu jukumu lake ndani ya uwanja lakini si vinginevyo,” alisema Sarri.

Akimzungumzia kiungo wake, Cesc Fabrigas, Sarri alisema anahitaji kumwona akiendelea kukaa katika klabu hiyo.

Kiungo huyo raia wa Hispania anadaiwa kuwa katika mipango ya kuondoka Ligi Kuu England lakini Sarri alisema amepanga kuzungumza naye kama ataweza kubadili mawazo yake.

Fabregas, David Luiz na Gary Cahill, mikataba yao inatarajia kumalizika majira ya joto yajayo lakini Sarri analazimika kuheshimu sera ya klabu ambayo inataka wachezaji wenye umri mkubwa kupewa mkataba wa mwaka mmoja.

 “Katika nafasi yao kuna wachezaji wawili tu, Jorginho na Febragas, hivyo upande wangu nahisi kutakuwa na tatizo kama nikimkosa Mhispania huyo,” alisema Sarri. “Nahitaji aendelee kuwapo, sifahamu uamuzi wa mwisho utakuwaje.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles