27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Sare za jeshi zasimamisha vigogo kazi

ANDREW MSECHU

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewasimamisha kazi viongozi watano wa Idara ya Huduma za Wakimbizi kwa kile alichodai ni kutokana na uzembe uliosababisha kuingizwa kwa sare za kijeshi katika kambi za wakimbizi Nduta iliyopo wilayani Kibondo na Mtendeli iliyopo wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Lugola aliwataja waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Harrison Mseke na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kwa Wakimbizi- Menejimenti ya Makambi na Makazi, Deusdedith Masusu.

Alisma wengine, ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma kwa Wakimbizi-Usalama na Oparesheni, Selemani Mziray, Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nduta, Peter Bulugu na Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Mtendeli, John Mwita.

“Pamoja na hao, ninaagiza Mratibu wa Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laizer achukuliwe hatua na mamlaka iliyoko juu yake haraka iwezekanavyo,” alisema.

Waziri Lugola, pia alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhan Kailima kuunda tume ya wataalamu ndani ya siku mbili kuchunguza tuhuma dhidi yao na taarifa ya tume hiyo iwe imewasilishwa kwake ndani ya siku 10 kuanzia jana.

Alisema amechukua hatua hiyo kutokana na ukweli kwamba kuingia kwa nguo hizo za kijeshi katika msaada uliotoka kwenye taasisi ya kimataifa ya Uniqlo nchini Japan kunaweza kuzorotesha uhusiano wa Tanzania na Burundi hasa kipindi hiki ambacho wanafanya jitihada za kurudisha wakimbizi nchini humo kutoka katika kambi hizo.

Alisema Burundi inaweza kuwa na wasiwasi kuwa wakimbizi hao wanaorudishwa kwao kwa hiyari wanapewa msaada wa kijeshi ili kujipanga wanaporudi kwao, suala ambalo linaweza kuifanya Serikali ya nchi hiyo kutokuwa tayari kuendelea na utaratibu wa kuwapokea kutokana na uzembe wa viongozi hao.

Alisema sare hizo 1,947, kati ya hio 1,325 zilikamatwa kwenye kambi ya Mtendeli na 622 Nduta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles