23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Sare na timu za Ligi Kuu zampa kichwa kocha Pamba

DAMIAN MASYENENE – MWANZA

MICHEZO miwili ya kirafiki ya Klabu ya Pamba, imeipa imani benchi la ufundi la timu hiyo ambalo linaamini sasa wachezaji wanafuata kile wanachoelekezwa.

Pamba inajiandaa na msimu mpya wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL).

Ili kujiweka sawa, Pamba imejipima dhidi ya Mbao FC na kuambulia sare ya mabao 2-2 kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Alliance, timu zote za zina maskani jijini Mwanza.

Kocha Mkuu wa Pamba, Muhibu Kanu aliliambia MTANZANIA kuwa,  kupitia michezo hiyo benchi lake la ufundi linaendelea kujifunza vitu vingi vitakavyoisaidia timu yake katika ushiriki wa FDL.

Alisema tayari, wamebaini makosa machache kwenye eneo la ulinzi na mlinda mlango, hivyo wataendelea kuyafanyia kazi, ambapo kesho wanatarajia kuivaa Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

“Bado tunajifunza vitu vingi kupitia michezo hii, kesho (Jana) tunacheza mchezo mwingine dhidi ya Toto Africans,  alafu tutakwenda Shinyanga kucheza na Mwadui.

“Hizi sare na timu za Ligi Kuu zinanipa nguvu kuona kile ninachokiingiza kwenye timu kinafanikiwa, wachezaji wangu wamecheza kwa moyo na kujitoa tuna makosa  madogo kwenye eneo la ulinzi na golikipa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles