28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Sare feki za jeshi zakamatwa kambi za wakimbizi Kigoma

Editha Karlo, Kigoma

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kibondo mkoani hapa, imekamata nguo zinazofanana za sare za kijeshi katika makambi ya wakimbizi.

Akizungumza na waandishi na kamati hiyo mjini hapa leo Alhamisi Januari 10, Kaimu Mkuu wa  Mkoa wa Kigoma, Samson Hanga, amesema nguo hizo zilikamatwa Desemba 31 mwaka jana kati saa tano asubuhi hadi sita mchana kwenye kwenye makambi ya wakimbizi.

“Jumla ya nguo zinazofanana na sare za kijeshi 1,947 zilikamatwa katika kambi ya wakimbizi ya Mtendeli na Nduta zote za hapa hapa Kigoma.

“Katika Kambi ya Nduta zilikamatwa sare 1,325 na Mtendeli 622,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaini walioingiza sare hizo na lengo lao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles