22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

SANGA: HATUNA URAFIKI NA YANGA

 

NA LULU RINGO


Mkurugenzi wa timu ya Singida United, Festo Sanga amesema timu ya Singida United inayoshiriki ligi kuu msimu huu si rafiki na klabu ya Yanga kama inavyozungumzwa na wengi.

Sanga alisema kumekuwa na minong’ono ya chinichini kihusu timu hiyo kuwa na urafiki na timu ya Yanga kutokana na kutoa wachezaji wake wawili, Deus Kaseke na Abdallah Salum (Fie toto) bila malipo kwenda Yanga.

Sanga aliwaambia waandishi wa habari kwamba klabu ya Singida united haijawahi kuwa na urafiki na Yanga na hautakuja kutokea na ndio maana kila mchezo wanaokutana nao huibuka washindi au sare.

“Kuwatoa wachezaji wetu bila malipo Yanga haimaanishi sisi ni marafiki, kila mechi tutakayocheza tutawafunga kama tulivyowafunga msimu ulioisha na katika mchezo wa FA,” alisema Mkurugenzi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,814FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles