27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

SAMUELS AMCHOKOZA NICKI MINAJ

Nicki MinajNEW YORK, MAREKANI

MPENZI wa zamani wa Nick Minaj, Safaree Samuels, amemchokoza mrembo huyo kwa kudai kwamba amemsaidia
sana kuandika nyimbo kali ambazo zimempa jina.

Samuels amesisitiza kwamba bila yeye Nick asingefika alipo, kwani mafanikio ya msanii huyo yametokana na kumwandikia nyimbo kali kama ‘Only’ambayo alimshirikisha Chris Brown, Drake na Lil Wayne, ‘Flawless’ ambaye
alimshirikisha Beyonce na ‘Feeling Myself’ aliomshirikisha Bey.

“Kila wakati nilikuwa nakaa naye na kumwandikia muziki, alikuwa hawezi kuandika mwenyewe bila mimi, lakini
naamini atajifanya amenisahau ila nimemfanya awe pale kwa sasa, japokuwa alikuwa ananifanya kama mfanyakazi
wake,” alisema Safaree.

Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, lakini waliachana mwaka 2014, ambapo Machi, mwaka
huu mrembo huyo aliamua kuweka wazi uhusiano wake na mkali wa Hip Hop, Meek Mill.
Nick hajajibu lolote kuhusiana na tuhuma hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles