29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Samia : Ushindi wa CCM ndiyo njia ya kulinda mapinduzi ya Z’bar, muungano

Na MWANDISHI WETU -UNGUJA

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Map- induzi (CCM) ,amesema ushindi wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ndio njia pe- kee ya kulinda Muungano na Map- induzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Alisema kila mwana CCM ana- takiwa kulinda tunu hizo zilizoasisi- wa na aliyekuwa Rais wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema hayo jana wakati aki- zungumza na Wajumbe wa Hal- mashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mjini katika ukumbi wa Mkoa huo uliopo Amani Unguja.

Akihitimisha ziara yake ya ki-

chama ya siku tatu katika mikoa minne ya CCM iliyopo Unguja, Sa- mia aliwambia viongozi hao kuwa suala la ushindi wa CCM linataki- wa kupewa kipaumbele.

Katika maelezo yake Samia, aliwataka wajumbe hao kuwa ma- kini katika kupitisha wagombea na kwamba wanapaswa kuzingatia kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya dola, uongozi na maadili.

Alisema kamati za siasa zinawapitisha wagombea na kwamba baadaye wanapokuja ka- tika nafasi za uongozi na kutowa- jibika wanalalamika kwa kudai kuwa hawaonekani majimboni na hawawajibiki.

“Mkishawapitisha hao wag- ombea ambao wanatumia fedha mnaanza kulalamika tangu aingie

amelitupa jimbo ndio kaja mara hii lakini hawa watu mnawapitisha wenyewe na sisi huku juu mmetu- letea na alama nzuri tunasema hawa ndio wanaoaminika kwenye kamati zao warudisheni,”alisema

Aliwataka wajipange vizuri katika kupitisha wagombea hao kuhakikisha wanafuata miongozo ya kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya dola na katiba ya chama katika kuwapata wagombea.

Alisema kwa kuzingatia mion- gozo hiyo itasaidia kuwapata wag- ombea wenye sifa za kuwatumikia wananchi na kwamba kufuata mis- ingi hiyo ni vigumu sana kuwapata wagombea ambao wanaotumia rushwa ndani ya chama.

“Huu ndio muda wa kuzisoma kwa kina kanuni hizo ili mzijue

na ikifika muda muweze kufanya maamuzi sahihi yatakayosaidia vi- kao vya juu kutoa kurejesha watu wenye sifa zinazoendana na ma- takwa ya wananchi”, alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja, Talib Ali Talib alisema umejipanga kuhakikisha wanashinda na majim- bo yote yanakwenda CCM.

Alisema uongozi wa mkoa huo umejipanga na makundi mbalim- bali ya jumuiya za chama ili kuji- panga yema kwa jailli ya uchaguzi mkuu kwa lengo la kuipatia ushindi wa kishindo CCM.

Naye Katibu wa CCM mkoa huo, Abdallah Mwinyi akisoma taarifa ya kazi za chama na jumuiya, alieleza kuwa wanashirikiana vizuri na jumuiya zote za chama katika masuala mbali mbali ya kiutendaji.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles