30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Samia mgeni rasmi warsha ya uelewa wa viwanda kwa wanawake wa Kiislamu

Tunu Nassor -Dar es salaam

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika warsha ya siku moja ya uelewa wa viwanda kwa wanawake wa Kiislamu, itakayofanyika Januari 25 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema lengo la warsha hiyo ni kuwaonyesha fursa za viwanda wanawake, hasa wa Kiislamu.

Alisema Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Dar es Salaam limeona kuwapo haja ya kutoa mafunzo kwa wanawake ili wawe na uelewa mpana katika masuala ya viwanda.

“Ni imani ya baraza kuwa wanawake wengi watapata uelewa sahihi juu ya fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya viwanda nchini na kwa kujishugulisha na kufanya kazi ni ibada kwa mwanamke na mwanaume,” alisema Sheikh Salum.

Alisema warsha hiyo itashirikisha wanawake zaidi ya 3,000 hasa wa Kiislamu waliopo Mkoa wa Dar es Salaam.

“Mada mbalimbali zitatolewa na wadau wa uchumi wa viwanda wakiwamo Sido (Shirika la Viwanda Vidogo), TBS (Shirika la Viwango Tanzania), TIRDO (Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda), GS1 (kampuni inayotoa msimbomilia), TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) na NHIF (Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya),” alisema Sheikh Salum.

Aliongeza kuwa Tanzania ya viwanda itawezekana tu iwapo wanawake watashirikishwa katika uchumi huo na wao kushiriki kikamilifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles