30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

SAMIA AWATAKA WATAALAMU WAIHAKIKISHIE MAJI MUSOMA

NA SHOMARI BINDA


Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (Muwasa), Said Gantala, alipotembelea mradi mkubwa wa maji mjini humo juzi.Picha na Shomari Binda

MAKAMU wa Rais  ,Samia Suluhu Hassan, amewataka wataalamu wanaoshughulikia miundombinu ya maji kuiangalia kwa umakini   wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama mjini Musoma.

Kauli hiyo aliitoa  baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Mara kwa kutembelea miradi mbalimbali ukiwamo mradi mkubwa wa maji wenye uwezo wa kusambaza maji kwenye mji huo vikiwamo vijiji 21 vya Halmashauri ya Musoma Vijijini.

Akitembelea mradi huo uliopo eneo la Bukanga,  aliwaambia wataalamu   kwenye eneo la chujio la maji kuhakikisha wanakuwa makini katika shughuli zao.  

Akizungumzia suala la maji kwenye mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa shule ya msingi Mkendo, Samia alisema ameutembelea mradi huo na kujionea kazi kubwa iliyofanyika.

Makamu wa Rais alisema ni vema vyanzo vya maji vikalindwa na kutunzwa vizuri ili malengo ya kuwafikishia wananchi huduma hiyo yaweze kukamilika.  

"Nimetembelea na kuuona mradi mkubwa na mzuri wa maji utawezesha kupata maji safi na salama, naomba muutunze mradi  mji wa Musoma uweze kuwa na huduma hii kwa wakati wote na kutunufaisha," alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk.Vicent Naano, alisema mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi huu na kutoa huduma kwa asilimia 97 utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita 30,000 kwa siku wakati mahitaji ni lita 24,000 kwa siku.

Alisema  lita 10,000 za ziada kutoka kwenye mradi huo unaogharimu Sh  bilioni 45 zitasambazwa kwenye vijiji 21 vya  Musoma vijijini.

 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Muwasa), Said Gantala, alisema   mradi huo upo hatua za mwisho kukamilishwa.

Kabla ya kutembelea mradi huo wa maji, Makamu wa Rais alitembelea pia alitembelea shamba darasa la kilimo cha mbegu za muhogo kinachofanywa na J.K.T, Rwamkoma.

Mingine ni Hospitali ya Rufaa ya Mwalimu Nyerere iliyopo Manispaa ya Musoma   na ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya kiliometa 9 katika Manispaa ya Musoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles