27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SAMIA AMPA MTIHANI KAMISHNA MKUU TRA

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, ahakikishe anaweka utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara, kama njia ya kujadili na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Agizo hilo alilitoa jana Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu Kichere kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa maendeleo ya taifa.

Samia ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya maofisa wa TRA kuwanyanyasa wafanyabiashara na wengine kuwabambikizia kodi kubwa hali ambayo inazua malalamiko mengi jambo ambalo alisema ni muhimu likatafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

“Ni muhimu kama TRA itafanya mabadiliko yoyote ya ulipaji wa kodi, ikawafahamisha wafanyabiashara hao mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kutokea katika ulipaji wa kodi pindi wanapoagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha ulipaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa unafanyika kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu na sio kuwakandamiza Watanzania kwa kuwalipiza kodi mara mbili jambo ambalo halifai hata kidogo,” alisema Samia.

Pamoja na hali hiyo alimtaka Kichere kukomesha mara moja tabia ya baadhi ya maofisa wa mamlaka hiyo kutoa lugha chafu na kuudhi kwa wafanyabiashara, bali watumie lugha nzuri ili kuwahamasisha kulipa kodi kwa hiyari bila kulazimishwa na mtu.

Kwa upande wake, Kichere amemuahidi Makamu wa Rais kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha malalamiko mbalimbali yanayotolewa na wafanyabiashara yanapata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles