25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Samia ahimiza wanawake kuchangamkia fursa

MWANDISHI WETU -SIMIYU

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake wajasiriamali kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB hususani mikopo ya WAFI kukuza na kuboresha biashara zao.

Alisema hayo  jana, alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu.

“Niwahamasishe wakinamama kuchangamkia fursa hii inayotolewa na Benki ya CRDB. Mikopo hii ya WAFI itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya mtaji ambayo wakinamama wajasiriamali wamekuwa wakikumbana nayo,” alisema 

Aliitaka benki kuboresha vigezo vya upatikanaji wa mikopo hiyo ili kuwapa wanawake wengi zaidi fursa ya kupata mikopo hiyo.

 Meneja wa Kanda ya Ziwa Benki ya benki hiyo, Lusing Sitta alisema mpaka sasa imetoa mikopo ya zaidi ya Sh bilioni 500 kwa wajasiriamali wanawake.

 “Tunajivunia kuona muitikio wa wanawake wajasiriamali katika mikopo hii ni mkubwa. Lengo letu nikuona tunamuinua wanawake na kuwawezesha kuboresha biashara zao na kushindana katika soko,” alisema Sitta.

Alisema imefanikiwa kuingiza sokoni bidhaa na huduma maalumu kwaajili ya wakinamama ikiwemo Akaunti ya Malikia na huduma za bima za Lady Jubilee.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela alisema inachukulia kwa umuhimu suala la kumuwezesha mwanamke na ndio maana wametoa kipaumbele cha ajira kwa wanawake katika ngazi mbalimbali. 

“Asilimia 46 ya wafanyakazi wa Benki ni wanawake, na tunatamani kuona tunaongeza kufikia asilimia 50,” alisema Nsekela.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles