33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Samia adai Watanzania wachache wanapata elimu ya juu

Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema idadi ya Watanzania wanaopata elimu ya juu, ni ndogo  kulinganisha na nchi za jirani.

Kutokana na hali hiyo, ameiagiza Wizara ya Elimu na Ufundi kuweka mikakati ya kuongeza idadi ya wanaodahiliwa.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu cha St Joseph katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi, Profesa James Mdoe.

Alisema wizara hiyo, inapaswa kukaa na kuweka mikakati kwa kushirikiana na vyuo binafsi ambavyo ni mdau mkubwa wa serikali katika kuongeza udahili na kuboresha elimu ya juu.

Alisema asilimia 25 ya wahitimu wanaohitimu vyuo vikuu kila mwaka, wanatoka vyuo vikuu binafsi, hivyo wizara ikishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), inapaswa kuweka mikakati ya kuviwezesha kukua na kuongeza udahili.

“Kazi kubwa ya TCU inapaswa  kuvilea na kuvijengea uwezo vyuo vikuu kama St Joseph na isionekane ipo kwa ajili ya kuvifungua tu kwasababu, vyuo ni mbia muhimu wa Serikali,” alisema Profesa Mdoe.

“Najua mliwahi kufungiwa na TCU kwenye baadhi ya kozi kutokana na kasoro zilizokuwapo wakati huo,nafurahi na kufarijika kuona mlifanya marekebisho makubwa na kuendelea na ubora wenu na ujio wangu hapa, ni ushahidi Serikali imeridhika na maboresho ambayo mmeyafanya,” alisema

Alisema anataarifa tangu chuo hicho kianzishwe mwaka 2004, kimefanikiwa kutoa wahitimu 7,900 wa fani za uhandisi, ualimu wa sayansi na shahada katika fani mbalimbali.

Alisifu mchango wa Kanisa Katoliki katika utoaji wa elimu ya juu, kwani ilikuwa ya kwanza kuitikia wito wa Serikali kwa wadau binafsi miaka ya 1980 kuunga mkono juhudi za serikali katika kuanzisha vyuo vikuu hapa nchini.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Innocent Ngalinda, aliishukuru Serikali kwa namna inavyokiunga mkono chuo hicho kwa kuwapatia mikopo wanafunzi wanaojiunga nacho na kisha kuwapa ajira wahitimu wake.

Alisema chuo kimejidhatiti kuhakikisha kinatoa wahitimu ambao watamudu kujiajiri na kuajiri wenzao badala ya kusubiri ajira hivyo kutoa mchango wao kuifikisha Tanzania kwenye ndoto yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na wa viwanda.

“Safari ya kitaaluma siyo nyepesi sana ila nawashukuru wahadhiri wamewaandaa wahitimu na wameiva tayari kwenda kuitumikia jamii hivyo mkafanye kazi kwa ubunifu, weledi, mjitume na msijihusishe na rushwa ili watu watakapowaona wajue kwamba kweli nyinyi ni wahitimu wa Chuo Kikuu cha St Joseph,” alisema Profesa

“Someni wala msidhani mmefika mwisho, jifunzeni mambo mapya kila wakati na mhakikishe mnakuwa na nidhamu ya hali ya juu kwenye kazi zenu maana hiyo ndiyo siri ya mafanikio sehemu za kazi,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles