27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Samia aahidi ujenzi wa mabwawa

Pg 2 sept 1Patricia Kimelemeta, Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), kimeahidi kujenga mabwawa makubwa ya maji ili kuondoa tatizo la maji lililopo mkoani hapa.

Akizungumza wakati  wa mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Bahi mkoani Dodoma jana, mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan alisema  uamuzi huo unalenga kumaliza kero ya maji ya muda mrefu ambayo imesababisha wananchi kukosa huduma hiyo.

Alisema kutokana na matatizo ya ukame yaliyopo katika mkoa huo, Serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa na chama hicho italazimika kujenga mabwawa hayo ili kuhakikisha wananchi wanapata maji.

“Mkoa huu, ni miongoni mwa mikoa yenye ukame, tumeamua kujenga mabwawa katika baadhi ya maeneo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji,”alisema Samia.

Katika mkakati huo pia, chama hicho kimeahidi kujenga mabweni ya shule za sekondari ili wanafunzi hasa wa kike waweze kusoma katika mazingira mazuri kuepuka kupata mimba.

Alisema  kwa kujenga mabweni, wanafunzi hao wataweza kujiepusha na vishawishi vitakavyojitokeza katika maeneo yanayowazunguka, jambo ambalo linaweza kusaidia kumalizika masomo yao.

Hata hivyo, mgombea huyo alisema  chama hicho kimepanga kujenga viwanda vidogo vya kuchakata ubuyu na karanga ili waweze kuuza ndani na nje ya nchi.

Alisema, ikiwa viwanda hivyo vitajenga, wataondoa tatizo la ajira kwa wakazi wa eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles