26.5 C
Dar es Salaam
Thursday, January 27, 2022

SAMIA AAGIZA WAKANDARASI WA NDANI WAPEWE ZABUNI

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa mwaka wa mashauriano wa wakandarasi ulioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) mjini Dodoma jana.

 

 

 

Na Mwandishi Wetu,

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe wakandarasi wa ndani hasa kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani.

Alisema hatua hiyo, itasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na  uwekezaji ndani ya nchi.

Samia,alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana, wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi wa mwaka 2017.

Aliwataka wakandarasi kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili, sheria  na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda uliopangwa kwa kuzingatia ubora na gharama zilizokubalika kwenye mikataba na si vinginevyo.

Aliwaasa kuacha mara moja tabia ya kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wanayopewa.

Alisema Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubutu kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwa kufanya hivyo kutaleta faida mbalimbali, ikiwamo fedha watakazopata watawekeza ndani ya nchi na kutoa ajira za kutosha.

Kuhusu madeni, aliwahakikishia kuwa Serikali haijawasahau na bajeti ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambayo imepitishwa na Bunge, imezingatia kilio chao.

Alisema Srikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa ili kujenga uhusiano mzuri uliopo.

Naye Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisisitiza kuwa wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na maadili kwa wakandarasi ili kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa kote, inakuwa na ubora unaotakiwa.

Naye Msajili wa Bodi ya Wakandarasi, Rhoben Nkori alisema bodi hiyo imefuta usajili wa wakandarasi 3,000 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya  usajili wa wakandarasi ya mwaka 1997.Kwa sasa bodi hiyo ina wakandarasi 9,000.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,803FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles