25.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 30, 2022

Contact us: [email protected]

Samatta, Wanyama waguswa maafa ya tetemeko Bukoba, watuma salamu za pole

sammata-na-wanyama

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

NAHODHA wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ anayekipiga katika klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, ameguswa na kutoa pole kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 17.

Samatta alionyesha kuguswa na tukio hilo baada ya kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twiter, kuwapa pole wakazi wa Bukoba waliopoteza maisha katika tukio hilo.

“Poleni wakazi wa Bukoba kwa kupoteza ndugu, jamaa na marafiki pamoja na mali, tunawaombea Mungu waliotangulia mbele ya haki wapumzike kwa amani,” aliandika mchezaji huyo Mtanzania.

Wakati huo huo, mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Kenya ambaye anakipiga katika Ligi Kuu ya Uingereza akichezea klabu ya Southampton, Victor Wanyama, naye alitoa pole kwa wahanga hao.

Mchezaji huyo ambaye naye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, aliandika kupitia ukurasa wake wa Twiter kwa kueleza kuwa anawapa pole Watanzania na kuwaombea wote ambao wamekumbwa na janga hilo.

“Maombi yangu ni kwa ndugu zangu Tanzania hasa Bukoba, ambao wamekumbwa na janga kubwa la tetemeko la ardhi na kupoteza ndugu, jamaa na marafiki, tupo pamoja,” aliandika Wanyama.

Wachezaji hawa wameendelea kuitangaza vema Afrika Mashariki katika bara la Ulaya, kupitia timu wanazochezea kwa kuonyesha soka safi na la kuvutia na kufanikiwa kujizolea mashabiki wengi katika nchi hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles