25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Samatta kumfukuzisha kazi John Stones

LONDON, ENGLAND

BEKI wa kati wa timu ya Manchester City, John Stones, anaweza hasionekane akiwa na kikosi hicho msimu ujao baada ya juzi kushindwa kumzuia mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta.

Tukio hilo lilitokea kwenye fainali ya Kombe la Carabao ambapo mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Manchester City waliibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku bao moja la Aston Villa likifungwa na Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa Tanzania ‘Taifa Stars’

Bao hilo la Samatta lilifungwa baada ya Anwar El Ghazi kupiga pasi ya juu ikimlenga Samatta na Stones akijikuta anaanguka chini kwa urahisi.

Kitendo hicho kimewafanya mashabiki wa Manchester City kuja juu kupitia mitandao ya kijamii huku wakiutaka uongozi wa timu hiyo kuachana na mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu kutokana na uwezo wake kuwa dhaifu kwa siku za hivi karibuni.

Bao hilo la Samatta limewaaminisha mashabiki wa Manchester City kuwa Stones amefikia hatua ya mwisho ya kiwango chake ambacho hakiwezi kuisaidia timu hiyo kwenye michuano mbalimbali.

Wakati wa Januari mwaka huu Manchester City walikuwa kwenye mipango ya kutaka kuachana na mchezaji huyo kwa kumrudisha katika klabu yake ya zamani Everton kwa kubadilishana na Mason Holgate.

Samatta amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka kwa Tanzania na kucheza fainali ya Kombe la Carabao, lakini amekuwa mchezaji wa kwanza kucheza kwenye Uwanja wa Wembley.

Mchezaji huyo amejiunga na Aston Villa wakati wa uhamisho wa dirisha dogo la usajili wa Januari akitokea KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji. Baada ya mchezo huo wa juzi Aston Villa wanazihamishia nguvu zao kwenye michezo ya Ligi Kuu nchini England kwa ajili ya kujikwamua kwenye kushuk

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles