23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Samatta afunguka kumrithi Lukaku

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta, amesema yupo tayari kukipiga Manchester United na kurithi sawa sawa nafasi ya  Romeru Lukaku, endapo ataondoka Old Trafford.

Samatta alimaliza kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya nchini Ubelgiji, baada ya kufunga mabao 23 huku pia akiiwezesha timu yake ya KRC Gekng  kutwaa ubingwa.

Kutokana na mafanikio yake hayo, Samatta ambaye alijiunga na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kimemokrasia ya Kongo(DRC), amekuwa akidaiwa kunyatiwa na klabu kadhaa zinazoshiriki Ligi Kuu England.

Pia anahusishwa na kwenda  kuchukua nafasi ya Lukaku ambaye ameonyeshwa mlango wa kutokea Manchester United, ingawa hakuna taarifa rasmi zilizotolewa na klabu hizo mbili mpaka sasa.

Akizungumza juzi baada ya kumalizika kwa mchezo wa hisani kati ya Team Samatta na Team Kiba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Samatta alisema anaamini anaweza kutakata akiwa na Mashetani hao wekundu kama atapata fursa ya kujiunga nao.

“Naweza kwenda kucheza Manchester, nilishawahi kuweka wazi kuwa naipenda Ligi ya Uingereza, japo mafanikio hayatakuwa kama ya Genk na presha itakuwa kubwa.Mpira ni ule ule, kwa sasa nafahamu mpira wa Ulaya ulivyo,” alisema Samatta ambaye alikuwa nahodha wa  Team Samatta iliyoshinda mabao 6-3 katika mchezo huo.

Samatta ambaye pia ni mshambuliaji wa zamani wa Simba alisema, anatamani kuhamia England, lakini haitakuwa tatizo kwake kuendelea kubakia Genk ikiwa  hatapata fursa nzuri itakayomfanya kuondoka  Ubelgiji.

Alipoulizwa kuhusu mtazamo wake baada ya timu  za mataifa mbalimbali kupiga kambi  sehemu mbali mbali hususani barani Ulaya kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon)ambayo imepangwa kuanza Juni 21 hadi 19 nchini Misri, nahodha huyo wa  Taifa Stars alisema, hilo haliwakatishi tama, badala yake watapambana kuhakikisha wanafanya vizuri.


“Kuna mchezaji mmoja wa zamani alishawahi kusema huwezi ukaweka begi la hela likacheza uwanjani, sisi tutafanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha tunang’ara katika michuano hiyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles