24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Samaki wanaotengeneza mchanga

samaki

Na William Shao,

Kuna vyanzo vingi mbalimbali vinavyotengeneza mchanga, lakinihuenda ukashangazwa na moja ya vyanzo vinavyoelezwa katika makala hii. Ni samaki anayesaga tumbawe na kuwa mchanga laini—samaki aina ya pono.

Pono (parrot fish) wanaishi katika maji ya kitropiki duniani pote. Baada ya kumeza kipande cha tumbawe, wanatafuta chembechembe za chakula na kutema mabaki, ambayo ni mchanga. Ili kufanya kazi yake, samaki huyo anatumia taya za midomo yake imara na meno yake magumu.

Ellen Wittlinger katika kitabu chake, ‘Parrotfish’, anaandika kuwa baadhi jamii za samaki hao wanaweza kuishi miaka 20 bila meno yake kupukutika.

Katika maeneo yenye matumbawe yaliyokufa, samaki huyo hutafuna kwa urahisi na

Kutengeneza mchanga kwa wingi kuliko chanzo kingine chochote cha asili. Watafiti fulani wanakadiria kwamba samaki huyo huzalisha mamia ya kilogramu za mchanga kwa mwaka.

Kwa mujibu wa waandishi Brandon Cole na Scott Michael katika kitabu chao, ‘Reef Life: A Guide to Tropical Marine Life’, Pono hufanya kazi nyingine muhimu. Anapokula matumbawe yaliyokufa, miani iliyo kwenye tumbawe na majani, jambo hilo hudumisha usafi wa tumbawe.

Tumbawe ni chakula muhimu kwa pono, na hii ndiyo sababu huyatunza matumbawe. Sehemu ambazo hakuna pono na viumbe wengine wanaofanya hivyo, matumbawe huharibiwa na miani na magugu-maji. “Wengine hudai kwamba matumbawe yaliyopo sasa yasingekuwa katika hali hiyo ikiwa kusingekuwa na viumbe kama hao,” kinaeleza kitabu ‘Reef Life’.

Wakati wa kulala, kinasema kitabu ‘Reef Life’, ili kuwa salama zaidi, baadhi ya samaki hao hujifunika wakati wa usiku. Wao hutoa ute wenye utelezi ambao hufunika kabisa miili yao, na kuwa kama gauni.

Wanasayansi wa viumbe vya majini wanaamini kwamba harufu mbaya inayotoka kwenye ute huo huwalinda kutoka kwa viumbe wanaowawinda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles