29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Samaki wa Ziwa Victoria sasa kuuzwa moja kwa moja Uholanzi

BENJAMIN MASESE-MWANZA

SERIKALI imepokea injini mbili kutoka Korea Kusini ambazo zitafungwa kwenye meli mpya ya MV Mwanza, huku ikizindua pia safari za ndege kusafirikisha minofu ya samaki kwenda nchini Uholanzi ambapo Shirika la ndege la Rwanda litakuwa likiisafirisha.

Mbali na kuzindua usafirishaji huo wa samaki, pia imetangaza kwamba sasa uwanja wa ndege wa Mwanza unakuwa wa kimataifa.

Meli

Akizungumza jijini Mwanza jana baada ya kuzindua safari za ndege na kupokea injini hizo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaack Kamwelwe, meli inayotengenezea jijini Mwanza itakuwa ikifanya za Mwanza-Bukoba na nchi jirani za Kenya na Uganda

Alisema meli hiyo inayogharimu Sh bilioni 159 inatarajia kukamilika na Januari 2021 na kuwataka wakandarasi  ambao ni  Gas Entec Co. Ltd, Kangnam Corporation zote kutoka Korea ya Kusini zikishirikiana na Suma JKT ya Tanzania kuhakikisha zinakamilisha shughuli hiyo  kama mkataba unavyoelekeza.

 “Meli hii itakuwa kubwa kuliko meli zote katika ukanda huu wa maziwa makuu, itakuwa na mita 92.6, kimo chake kitakuwa mita 11.2, upana mita 17 na uzito wa tani 3,500 kwa takwimu hizo ndio itakuwa meli kubwa kuliko zote na itakuwa inatumia masaa saba kutoka Mwanza hadi Bukoba,”alisema.

Akitoa ufafanuzi wa injini hizo, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania (MSCL), Erick Hamisi, alisema injini hizo zimenunuliwa kwa Dola za Marekani 39,000,000 sawa na Sh bilioni 89.764  na kila moja ina tani 35 na uwezo wa kuzaliza KW 2,380.

Alisema uwezo huo wa injini utaiwezesha meli hiyo kusafiri kwa saa sita kutoka Mwanza hadi Bukoba na kwamba hadi sasa wakandarasi hao wamelipwa Sh bilioni 55.618 sawa na asilimia 64 ya gharama zote.

“Kila injini itakuwa na uwezo wa kutumia mafuta lita 9,300 kutoka Mwanza hadi Bukoba, hivyo kwa injini mbili zitatumia lita 18,600  kwa kusafirisha abiria 1200, tani 400 za mizigo na magari madogo 20 lakini meli hii  itakuwa na madaraja sita, daraja la uchumi abiria 834, daraja la biashara abiria 200, darala la pili la kulala abiria 100, darala la kwanza abiria 60 na daraja la hadhi ya juu abiria wanne, mwisho ni VIP abiria wawili.

Safari za ndege

Katika hatua nyingine Kamwelwe alizindua safari za Mwanza hadi hadi Uholanzi katika kwa kutumia shirika la Ndege ya Rwanda ambapo  jana ilisafirishwa tani  nane za minofu ya samaki huku akifafanua kwamba kila wiki kutakuwa na safari moja.

Kutokana na safari hizo, amewaagiza wakuu wa mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu na Kagera kuunda mtandao wa pamoja wa kuhakikisha samaki wote wanaletwa kwenye viwanda ili kurahisisha upatikanaji wa minofu hiyo na kufikishwa uwanja wa kimataifa wa Mwanza.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles