23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

SAMAKI SASA KUUZWA KWENYE MABUCHA

 

samaki-ferry-3

CHRISTINA GAULUHANGA NA VERONICA ROMWALD-DAR ES SALAAM


 

SAMAKI wanaovuliwa katika Bahari ya Hindi sasa kuuzwa katika mabucha maalumu ya asamaki badala ya mitaani kama ilivyo sasa.

Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uvuvi wa Soko hilo, Victoria Mwandike alisema uongozi wa soko hilo uko kwenye mchakato wa kupendekeza hatua hiyo ili kuzuia uuzwaji holela wa samaki wapo samaki wanaouzwa mitaani hasa kwenye vituo vya mabasi na mitaani.

Pamoja na mambo mengine alisema zaidi ya tani 1.5 waliovuliwa kwa njia ya milipuko na baruti wamekamatwa katika soko la Kimataifa la Samaki Feri jijini Dar es Salaam.

Samaki hao walikamatwa wiki iliyopita katika msako maalumu kabla ya kuanza kusambazwa kwa wafanyabiashara kwa ajili ya kuuzwa.

“Bado tunafanya msako wa kukamata na kudhibiti uingizwaji wa samaki waliovuliwa kwa njia haramu, wiki iliyopita zilikamatwa tani 1.5 na mapema wiki hii tumekamata kilo 20,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo bado wanahimiza Watanzania kuwa makini kwani wavuvi hao wasiokuwa waaminifu wanaendelea kuingiza samaki hizo.

“Lakini kwa kuwa tunaimarisha mifumo yetu ya ndani ya soko sasa wanawauzia wafanyabiashara na wao wanakwenda kuwauza moja kwa moja huko mitaani, wavuvi waliokamatwa na maofisa hao tayari wamechukuliwa hatua za kisheria.

“Lakini ni vema sasa mamlaka zinazohusika na uuzwaji na usimamizi wa milipuko hasa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Kilimo na Mifugo na Jeshi la Polisi wadhibiti upatikanaji holela wa bidhaa hiyo ili tutokomeze uvuvi haramu ambao kwa sasa umekithiri katika Bahari ya Hindi,” alisema.

Alisema wavuvi baada ya kununua milipuko hiyo huipooza kwa kuchanganya na kemikali wanazozifahamu wao kisha huitumia kwa kuvua samaki.

“Zipo athari nyingi za uvuvi haramu lakini kikubwa eneo hilo hupoteza uhalisia wake kwa zaidi ya miaka 100  na baada ya hapo ndiyo huanza kurejea katika hali ya kawaida, jambo ambalo limesababisha hata samaki siku hizi samaki kupatikana maeneo ya mbali tofauti na zamani,”alisema Mwandike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles