24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

SAMAKI, DAGAA FERI BEI JUU

NA CHRISTINA GAULUHANGA–DAR ES SALAAM


BEI ya samaki na dagaa katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri imezidi kupanda kwa sababu ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa wadau wa soko hilo, Omary Mtolea, alisema kupanda kwa gharama hizo kunatokana na mvua nyingi  hivyo kusababisha samaki kupatikana kidogo tofauti na siku ambazo si za mvua.

Mtolea alisema hali hiyo imesababisha soko la bidhaa hiyo kuwa gumu kwa sababu wananchi wengi wanashindwa kumudu gharama hizo hasa wale wenye kipato cha chini.

“Kwa sasa baharini samaki na dagaa wanapatikana wachache ambao wamesababisha hata wavuvi kuuza kwa bei ya juu na kupandisha kwa kasi bei za bidhaa hizo,” alisema Mtolea.

Alisema awali bei ya dagaa ndoo moja ilikuwa inauzwa kati ya Sh15, 000 hadi 20,000, lakini  kwa sasa inauzwa kati ya Sh 20,000 hadi 50,000.

Mtolea alisema kwa upande wa ngulu maarufu ‘kingfish’, kwa sasa anauzwa Sh 50,000 wakati awali alikuwa akiuzwa Sh 30,000 hadi 20,000.

Pia samaki aina ya Redsnaper kwa sasa anauzwa kati ya Sh 55,000 hadi 70,000 wakati awali alikuwa akiuzwa Sh 30,000 hadi 40,000.

Mtolea aliongeza kuwa dagaa ambazo hupendwa na wateja wengi kwa sasa ndoo moja inauzwa kati ya Sh 20,000 hadi 30,000 wakati awali zilikuwa zikiuzwa Sh10, 000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles