33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SAMAHANI JAY MOE TUNAOMBA TUKUSAIDIE KUSHEA MISTARI

SIDHANI kama Darasa alipotoa ngoma yake ‘Muziki’ alitarajia kujifananisha na muoka mikate aliyeweka hamira kwenye mistari ya Kemo. Kwamba sasa Kemo imeumuka na ngoma nyingi zinatiririka na kusababisha mistari kuzimikiwa bila kujali kama ngoma zinazotemwa zimedhamiriwa kuifunika ngoma ya Darasa.

Au hamasa mpya kwenye mikong’osio hiyo inayotema cheche na kuhusudiwa sana. Lakini kwa mfano mwingine kwa upande wa kukimbiza hadi sasa Weusi ni kama mwanariadha Usain Bolt, bado mbinu zao zinawapa kasi kubwa wakiwa ‘Crew’ na kampuni lakini kuna mbabe mwingine wa Kemo aliyekuwa amekausha kwa kitambo aliyeibuka upya kwenye gemu.

Licha ya Jay Moe kuchana mistari ya kuponda kushea kwa ajili ya ‘promo’ lakini kwa ngoma yake ‘Nisaidie Kushea’ anastahili kusaidiwa kushea kwani kutoka ‘Back’ yake mwenyewe hadi ‘Front’ ya sasa uwezo wake uko vizuri kama kawaida yake siku zote.

Ukimtathmini Juma Mohamed Mchopanga a.k.a Mo Skills a.k.a Superman a.k.a Mo Genius a.k.a Jay Moe kwa muda mfupi tangu alipotema ‘Pesa ya Madafu’ licha ya kubaki kwenye misingi ya vina na mizani yenye mashiko ya Mc wa ukweli ‘ameji-brand’ vyema.

Ukimcheki kwenye vichupa vyake amepiga kama wale wanaokimbiza kwa kusoma gemu nd’o maana ya kuwafananisha Weusi na Usain Bolt ingawa walipoanza kujiweka kwa muonekano huo kuna ambao hawakuwasoma, lakini wametengeneza njia kama Darasa alivyotia hamira kwenye Kemo na sasa Jay Moe anaongeza ‘skills’ kwa kuishika gemu katika mtazamo wa muda uliopo sasa tofauti na mida ile ya ‘Back’ ya ngoma zake Bishoo, Jua na Mvua, Kama Unataka Demu, Maisha ya Boarding, Stori Tatu Tofauti’ na ‘Sihitaji’ akidhihirisha kwamba ukongwe ni dawa kwenye gemu.

Miaka 38 na ushei kiumri lakini pia miaka 19 kwenye gemu siyo michache kuwa na uwezo wa kufanya mambo makubwa, uzoefu ni muhimu pia na kama sasa ni wakati wa kushea hata kama Jay Moe huzimikii promo ya kushea, mashabiki lazima wakuombe samahani manake kichupa kipya ulichotema kinafaa kushea.

Kagua kichupa hicho, hata kama huna muda wa kufanya hivyo lakini lazima utakiona manake kwa sasa kinakimbiza sana kwenye kioo.

Kichupa kimekwenda shule, location imetulia, pamba zinavutia na ‘Video Vixens’ wenye mvuto adimu nd’o habari iliyomo ndani ya kichupa cha kushea na haihitaji kuombwa kusaidia kuusambaza manake ngoma iko poa, hata msanii mwenyewe pia amefanya poa na kichupa kimeongozwa poa.

Kwa kinachoibuka hivi sasa kwa Kemo kutema ngoma kali kila kukicha maana yake ni kwamba inazidi kukamata na kujiweka katika mashiko yake, nd’o maana ni vigumu kuiondoa kwenye ulingo kwani haihitaji kiki za kutengeneza kwa kujisambaza yenyewe nd’o maana ya chema chajiuza bila mbinu mbadala.

Kwa spidi yako ya sasa Jay Moe si tu kukusaidia kushea, lakini katika ‘Front’ ya Kemo kukomaa na kupagawisha mashabiki tunakusaidia kukushauri pia kwamba usipige zile za kuibuka na kupotea, ibuka na kukomalia gemu bila kuachia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles