23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Sam wa Ukweli: Mkataba ulinibana

sm-pic

NA BEATRICE KAIZA,

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Salim Mohamed ‘Sam wa Ukweli’,  amesema sababu zilizomfanya kukaa kimya kwa muda mrefu ni kutokana na kubanwa na mkataba.

Akizungumza na MTANZANIA, alisema  baada ya kutoka Emotion Record alijiunga na Al jazeera Entertainment, lakini alishindwa kuwa huru kufanya kazi zake kutokana na kubanwa na mkataba ambao aliusaini.

“Nilitaka kuvunjwa mkataba na lebo ya Al jazeera kutokana na kuona hakuna kazi iliyokuwa inafanyika, hivyo nilitaka kuwa huru lakini ilishindikana na niliambiwa nilipe Sh milioni 100 kama nataka kutoka kwenye lebo hiyo, hali hiyo ilinifanya nikae kimya kwa muda mrefu,” alisema Sam wa Ukweli.

Aliongezea kuwa kwa sasa mkataba umekwisha na yuko huru kufanya kazi na mtu yeyote na anatarajia kuachia ngoma, kwa sasa anatamba na wimbo wake ujulikanao ‘Kisiki’ na kuwaomba mashabiki zake kumpokea kwa moyo mmoja kwa kurejea tena kwenye tasnia ya muziki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles