SALMAN KHAN APATA DHAMANA

0
1032

JODHPUR, INDIA


MWIGIZAJI bora wa filamu za Bollywood, Salman Khan, amepewa dhamana baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano.

Msanii huyo alihukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kosa la kuua aina mojawapo ya swala ambao ni adimu kupatikana duniani, tukio lililotokea mwaka 1988.

Mahakama hiyo iliyopo Jodhpur nchini India, ilimpa hukumu hiyo na kumtoza faini ya rupia 10,000 sawa na dola 154 au pauni 109, ambazo ni sawa na 347,124 za Kitanzania, lakini msanii huyo tayari amepata dhamana juzi.

Inasemekana kuwa Khan mwenye umri wa miaka 52, aliua swala wawili ambao walikuwa kwenye hifadhi ya Rajasthan wakati akitengeneza filamu yake.

Kundi kubwa la watu lilikusanyika nje ya gereza juzi wakiwa wanacheza, wakipiga kelele na kuimba mara baada ya kupata taarifa kwamba anaweza kuachiwa huru. Hata hivyo, wasanii wenzake wanne ambao walikuwa pamoja wakati wa utengenezaji wa filamu hiyo ya Hum Saath Hain, walikutwa hawana hatia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here