26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

SAKAYA: TAKUKURU INIHOJI MIMI FEDHA ZA RUZUKU, SI MAALIM SEIF

Elizabeth Hombo, Dodoma         |          


Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF) amesema Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) imhoji yeye  kuhusu fedha za chama hicho kutopelekwa kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) badala ya Maalim Seif Sharif Hamad.

Sakaya ametoa kauli hiyo leo bungeni akijibu hoja ya Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji ambaye alitaka Maalim Seif ahojiwe kwa kutopeleka hesabu za CUF kwa CAG.

“Khatib kasema Maalim ahojiwe wakati yeye hayuko ofisini tangu mwaka jana. Suala la ruzuku ya chama anatakiwa ahojiwe Sakaya ambaye ndiye anayekaimu nafasi ya Katibu Mkuu.

“Takukuru inihoji mimi maana ndiye najua mambo ya ofisi ya CUF maana huwezi kujua mambo ya ofisini kama uko mitaani,” amesema.

Leo asubuhi wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha, Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Ally alilitaka Bunge kuamuru, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif ahojiwe na Takukuru kwa kutopeleka hesabu za fedha za chama kukaguliwa na CAG.

Khatibu alisema Katibu Mkuu huyo, hajakitendea haki chama kwa kutopeleka mahesabu kwa CAG, kauli iliyoungwa mkono na Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye alisema; “katika jambo hilo tunakuunga mkono kwa kuwa ni la maana.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles