Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA |
UHABA wa mafuta ya kula unaodaiwa kuikumba baadhi ya mikoa nchini, umetikisa Bunge huku baadhi ya wabunge wa CCM wakitaka maelezo ya Serikali kuhusu suala hilo.
Kwa mara ya kwanza sakata hilo liliibuliwa bungeni wiki iliyopita na Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema), ambaye aliomba mwongozi wa Spika kutokana na kuadimika kwa biadhaa hiyo.
Mafuta ya kula yameripotiwa kuadimika katika maeneo mbalimbali mikoani na jana suala hilo lilichukua sura mpya, ambapo wabunge wa CCM walihoji tena uwepo wa taarifa za kuadimika kwa bidhaa hiyo.
Wabunge wa CCM, Juma Nkamia (Chemba) na mwenzake Hussein Bashe (Nzega Mjini), walisimama na kuomba mwongozo kutokana na kuadimika kwa mafuta ya kula nchini.
Katika mwongozo wake Nkamia, alisema vyombo vya habari hususan magazeti yameandika kuhusiana na kuadimika kwa mafuta ya kula.
“Leo (jana) mheshimiwa waziri wakati akijibu swali namba 190 la mheshimiwa Costantine Kanyasu kuhusiana na suala la Pamba nilikuwa naomba mwongozo wako mbegu za Pamba ni miongoni mwa mbegu ambazo zinatoa mafuta ya kula.
“Kuanzia jana (juzi) na leo (jana), vyombo vingi vya habari hasa magazeti vimekuwa vikiandika juu ya kuadimika kwa mafuta ya kula hapa nchini hali ambayo inasababisha mafuta …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.