27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kutekwa Mo Dewji: Mahakama yatoa hati raia watano wa kigeni kukamatwa

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kuwakamata raia wanne wa Msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini wafikishwe kizimbani kuunganishwa katika mashtaka ya kumteka Mohammed Dewji.

Mahakama imetoa hati hiyo leo Jumanne Julai 23,   mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuomba kufanya hivyo.

Wankyo aliwataja wanaosakwa kuunganishwa na Mshtakiwa  Mousa Twaleb (46) ni raia wa Msumbiji, Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issa Tomo, Zacarious Junior na raia wa Afrika Kusini Phila Tshabalala.

Washtakiwa hao wanatakiwa kuunganishwa katika shtaka la pili na shtaka la tatu ambapo shtaka la kwanza linamkabili Twaleb ambaye anadaiwa  kujihusisha na genge la uhalifu,  kati ya Mei mosi mwaka 2018 na Oktoba mwaka huo Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Johannesburg Afrika Kusini.

Inadaiwa shtaka la pili la kujihusisha na genge la uhalifu linamuhusu washtakiwa wote wanaosakwa ili wafikishwe mahakamani.

Shtaka la tatu washtakiwa wote wanadaiwa kuteka nyara, inadaiwa Oktoba 11 mwaka 2018 katika Hoteli ya Colleseum wilayani Kinondoni, akiwa pamoja na wenzake walimteka mfanyabiashara, Mohammed Dewji kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri kinyume cha sheria.

Mshtakiwa Twaleb katika shtaka la nne wanadaiwa kutakatisha fedha Sh milioni nane, inadaiwa Julai 10 mwaka jana maeneo ya Mbezi Beach alijipatia kiasi hicho cha fedha huku akijua fedha hizo ni mazalia ya genge la uhalifu. Kesi itatajwa Agosti 6 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles