27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Sakata la Greenland lamfanya Trump avunje safari ya Denmark

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump amefutilia mbali ziara yake rasmi nchini Denmark baada ya waziri mkuu wa taifa hilo kusema Greenland haitauziwa Marekani.

Rais huyo alitarajiwa kuzuru Dernmark, Septemba 2 kwa mwaliko wa malkia wa taifa hilo Margrethe II.

Wiki iliopita Trump alikaririwa akisema Marekani ilikuwa na hamu kukinunua kisiwa kinachojitawala cha Greenland, Denmark.

Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen alisema mpango huo ni upuuzi na kusema kwamba alitumaini Trump hakulichukulia suala hilo na uzito mkubwa.

Akitangaza kuvunja safari yake Trump alituma ujumbe kupitia akaunti yake ya twitter akisema:

Denmark ni taifa maalum lenye watu wazuri sana lakini kutokana na matamshi ya waziri mkuu Mette Frederiksen hatakuwa na hamu ya kuzumngumzia ununuzi wa Greenland na ataahirisha mkutano wake uliopangwa wiki mbili zijazo hadi wakati mwingine.

Msemaji wa Ikulu ya Whitehouse alithibitisha kwamba ziara hiyo ya rais imefutiliwa mbali.

Rais huyo awali alikuwa amethibitisha ripoti kwamba alikuwa na hamu ya kununua kisiwa hucho cha Greenland.

Alipoulizwa siku ya Jumapili iwapo anaweza kuuza ardhi ya Marekani ili kununua kisiwa kwengineko, alisema kweli vitu vingi vinaweza kufanyika.

”Greenland ina utajiri wa madini, maji safi zaidi na barafu, samaki, chakula cha baharini kawi na ni kivutio kikuu cha utalii. Tuko wazi kwa biashara lakini sio kuuzwa”, ilisema wizara ya mambo yanje katika taarifa yake iliotumwa katika mitandao ya kijamii.

Waziri mkuu wa Greenland Kim Kielsen alirejelea matamshi yake katika taarifa nyingine tofauti .

”Greenland haiuzwi lakini iko wazi kibiashara na ushirikiano na mataifa mengine”, ilisema taarifa.

Greenland ndio kisiwa kikubwa zaidi duniani baada ya Australia ambayo inajulikana kama bara.

Kisiwa hicho kina takriban watu 56,000 walio na makaazi yao katika pwani yake.

Takriban asilimia 90 ni raia wa Greenland . Ina serikali yake na bunge lake.

Asilimia 80 ya kisiwa hicho imefunikwa na barafu ambayo inahofiwa kuyeyuka kutokana na viwango vya joto duniani.

Kuyeyuka kwa barafu hiyo kumesaidia katika utafutaji wa madini katika ardhi ya kisiwa hicho.

Lakini inaaminika kwamba kuyeyuka kwa barafu hiyo kunaweza kusababisha madhara yanayotokana na mabaki ya kinyuklia yaliowachwa katika kambi kadhaa za jeshi la Marekani wakati wa vita baridi.

Trump ameripotiwa kuvutiwa na kisiwa hicho kutokana na madini yake kama vile makaa, Zinc, Shaba na Chuma.

Pamoja na Greenland kuwa na utajiri wa maliasili, inategemea Denmark kwa theluthi mbili za mapato yake .

Ina viwango vya juu vya watu kujitoa uhai, ulevi wa pombe na ukosefu wa ajira.

Marekani imekuwa ikikiona kisiwa hicho kama eneo muhimu la kimkakati na iliweka kambi ya wanahewa wake mbali na rada yake wakati wa vita baridi

Wazo la kuinunua Greenland kwa mara ya kwanza liliwasilishwa 1860 chini ya urais wa Andrew Johnson.

Mwaka 1867 ripoti ya idara ya kigeni ilipendekeza kwamba eneo la kimkakati la Greenland pamoja na mali yake asili ni muhimu kulinunua.

Lakini hakuna hatua rasmi iliochukuliwa hadi 1946 , wakati Harry Truman aliipatia Denmark Dola milioni 100 kununua eneo hilo.

Alikuwa amewasilisha mpango wa kutaka kubadilishana ardhi ya Alaska na Greenland kulingana na shirika la habari la AP.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles