25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

Sakata la Escrow: Dk. Abbasi asema Serikali haidaiwi

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi, amesema Serikali haihusiki na hukumu iliyotolewa na Baraza la Kimataifa la Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICSID), ambayo imetaka Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) Ltd ilipwe dola za Marekani milioni 185. 

Akizungumzia hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 9, mwaka huu, Dk. Abbasi alisema amekuwa akiulizwa kuhusu hukumu hiyo, hivyo analazimika kutoa ufafanuzi.

“Msingi wa kesi zote mdaiwa si Serikali wala Tanesco, ni deni la benki dhidi ya IPTL (kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited) walilorithi miaka mingi kutoka wakopeshaji wa Malaysia.

“Kwa muktadha huo na kisheria, Serikali na Tanesco ziliunganishwa tu kama kanuni za kisheria zinavyomruhusu mdai kuwaunganisha wahusika wengine kwenye kesi ili kupata uhakika kuwa analipwa madai yake.

“Kwa muktadha huo, natumia fursa hii kuwatoa wasiwasi Watanzania, Serikali haidawi, haijawahi kukopa Standard Chartered ya Hong Kong, ila kama Baraza la Usuluhishi lilivyoamua, tutahakikisha tunasimamia utawala wa sheria kwa kuona IPTL wanalipa deni lao,” alisema.

Katika kesi hiyo ya ICSID yenye namba ARB/15/41, benki hiyo ilifungua kesi dhidi ya Serikali ikidai kiasi hicho cha fedha kwa kile ilichodai ni kutokana na kukiukwa kwa mkataba wa manunuzi ya umeme uliokuwa umetiwa saini baina yao na pande tatu za mkataba huo.

Benki hiyo ilikuwa ikiwakilishwa na Matthew Weiniger wa QC Linklaters LLP One, Iain Maxwell, Aaron McDonald, Elizabeth Kantor, Harry Ormsby, Gavin Creelman na Herbert Smith wa Freehills LLP, wote kutoka Uingereza. 

Hukumu hiyo inaonyesha Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Clement Mashamba, Beredy Malegesi wa Crax Law Partners, Richard Karumuna Rweyongeza wa R. K. Rweyongeza & Co. Advocates, Galileo Pozzoli, Mark Handley, Profesa Tullio Treves, Luciana Ricart, Irene Petrelli, Renato Treves na Valerio Salvatori Curtis wa Mallet-Prevost, Colt & Mosle LLP. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles