FRANCIS GODWIN,IRINGA
WANANCHI wa vijiji sita za kata ya Image Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, wametakiwa kuendelea kuwasaidia watoto wa kike na wajane kuwa na haki sawa ya kumiliki ardhi na mali nyingine katika familia bila kubaguliwa .
Rai hiyo imetolewa jana na mwezeshaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya Iringa Civil Society Organization (ICISO), inayojihusisha na masuala ya elimu kwa jamii juu ya umiliki wa ardhi ya mali kwa watoto wa kike.
Wakizungumza na wananchi wa kijiji cha Iyai, Mwezeshaji wa Shirika la ICISO, Ahazi Sibale alisema baadhi ya maeneo kumekuwapo na ubaguzi mkubwa kwa watoto wa kike kuingia katika orodha ya mgawanyo wa mahali za familia kutokana na utamaduni wa ovyo kuwa mtoto wa kike hapaswi kupewa mahali kwenye familia yake kwa kuwa anakwenda kuolewa .
” Wanaume wamekuwa wakielimishwa namna na kuandika wosia mapema ili kila mtoto kwenye familia ajue sehemu ya mali yake badala ya kukaa kimya na siku kifo kikitokea familia nyuma inaanza kunyanyasika,” alisema Sibale
Alisema kutokana na ubaguzi huo, shirika lake kwa kushirikiana na kwa kushirikiana na The Foundation for Civil Society walianza kazi ya kutoa elimu kwa wananchi wa baadhi ya kata za wilaya ya Iringa na Kilolo mkoani Iringa ili kupunguza ama kumaliza ubaguzi uliokuwepo dhidi ya watoto wa kike kutengwa katika umiliki wa mahali mbali mbali .
Alisema elimu hiyo, imeendelea kuwaamusha wanawake kuanza kufuatilia haki zao kwenye famili za kupewa mgawanyo sawa na wanaume katika mali mbali mbali na kwenye ardhi na sasa jamii baadhi ya maeneo inawapa haki sawa watoto wa kiume na wanawake katika mgawanyo wowote wa mali za kifamilia.
Alisema Kata ya Image, zaidi ya wananchi 100 wamefikiwa na elimu hiyo kwa ngazi ya kijiji na wapo waliopewa elimu ngazi ya kata namna ya kuwawezesha wanawake kuanzisha vikundi vya kiuchumi ili kuondokana na kuwa tegemezi katika familia.