29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Sahel Trading Co. waagizaji maarufu, wauzaji mizani Afrika Mashariki

AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

MIZANI si bidhaa kama bidhaa zingine wala si biashara kama zilivyo biashara nyingine bali ni huduma wezeshi katika kupima na kujua uzito kama inavyohitaji sheria na hati ya uthibitisho wa kukidhi vigezo kwa mtoa huduma stahiki katika jamii.

Kuna vipimo vya aina nyingi lakini mizani ni mahsusi kwa upimaji uzito wa bidhaa kama kigezo cha biashara husika ni uzito wake. Bila mizani husika hakuna ufanyaji  biashara kihalali.

Ni maneno ya Ally Abdul Hazam ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Sahel Trading Co. Ltd ambao ni wauzaji na wasambazaji wa vipimo vya uzito, mizani ya aina zote. Wakulima huuza mazao yao kwa uzito hivyo ni muhimu kuwa na watoa huduma waaminifu kukwepesha dhuluma ya vipimo.

Kwa mujibu wa Hazam, kampuni ya Sahel waanzilishi wa kutoa huduma ya kuuza vipimo  vya uzito (mizani) nchini Tanzania  kwa upande wa sekta binafsi ambao kwa muda mrefu inatoa huduma hiyo kwa mujibu wa sheria  nchini Tanzania na katika nchi za jirani ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia, Malawi, Kenya, Mozambique, Rwanda na Burundi.

Watoa huduma ya kuuza vipimo (mizani) ni wachache sana nchini Tanzania ikilinganishwa na bidhaa nyingine kutokana na umakini wake na matumizi yake katika nyanja tofauti na maeneo tofauti jambo ambalo ni changamoto kwa nchi inavyoendelea kupiga hatua kuelekea uchumi wa viwanda ambao mizani haikwepeki katika shughuli zozote za uzalishaji ndani ya viwanda.

Kutokana na uhitaji wa huduma hiyo kwa Tanzania, mwandishi ameamua kufanya utafiti na kubaini kuwa wauzaji wa vipimo waliopo ni wachache ambao wamekuwa wazalendo kulihudumia Taifa mchana na usiku hususani katika maeneo ya biashara pale ambapo huduma ya mizani ina hitajika kwa wakati sanjari na kuifanyia marekebisho ya kitaalamu pale inapotokea tatizo la kiufundi.

Aina ya Mizani

Hazam anasema mizani ipo ya aina nyingi kulingana na uhitaji ambapo ipo mizani ya kupimia kemikali, kupimia wanyama (mifugo) kupimia maziwa na vyakula, ya kupimia samaki wanaovuliwa baharini ambayo ni lazima iwe na uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani (water proof) ili kuilinda na kutu itokanayo na maji baharini kadhalika mizani ya kupimia gesi, kupima magari na mizigo mizito.

Vipimo hivi vinatoka katika nchi tofauti ambavyo wanaviagiza kulingana na mahitaji ya mteja.

Mfano vipimo  (mizani ya mizigo mizito, makontena na magari inatoka nchini Italia na ile inayotumika  katika maduka makubwa ya bidhaa (supermarket) inatoka Korea  ya Kusini huku ya biashara ya rejareja ambayo inafahamika kwa  rika zote ikitoka nchini Marekani.

Huduma yoyote inapotolewa kwa jamii yoyote haikosi kuwa na changamoto kwa watoa huduma ya vipimo, changamoto yao kubwa ni kutoa huduma ya marekebisho ya vipimo (mizani) pale linapotokea tatizo la kiufundi kwa wakati.

Anaelezea Hazam juu ya hili kuwa mizani ikisumbua mfano wa kupima uzito wa magari pengine bandarini au katika vituo vya magari, inawachukua muda kufika jambo ambalo linasababisha msongomano wa magari na kukwamisha shughuli za kimaendeleo.

Kutokana na uchache wao, hawajaweza kufanikiwa kuwa na wahandisi wa shughuli ya marekebisho  na ukarabati wa vipimo nchi nzima licha ya Wakala wa      Vipimo Tanzania kuwapa ushirikiano mkubwa juu ya hili.

Wakala wa Vipimo Tanzania katika harakati za kumaliza changamoto ya mizani kuharibika ghafla wameanzisha  programu ya kuzunguka nchi nzima na kutoa elimu ya utunzaji kwa wamiliki wa vipimo hivyo.

Hazam anadadavua kuwa mizani (vipimo) ambavyo vinatengenezwa nyakati hizi ni ya kisasa na haisumbui katika matumizi kama ilivokuwa miaka ya nyuma.

“Mizani inayotengezwa wakati huu mteja anarekebisha mwenyewe pale ambapo tatizo linatokea, biashara ya mizani imebaki kuwa huduma kutokana na kwamba sio kama chakula ambacho ni lazima mtu apate kila siku,” kwa mujibu wa watoa huduma hiyo akiwemo mkongwe kampuni ya SAHEL.

“Mwaka huu 2019, kampuni ya Sahel Trading Co. Ltd imejiboresha kwa kusambaza vipimo (mizani) ya kidigitali isiyohitaji umeme wala kuchaji ambayo imetengenezwa kisasa zaidi kulingana na maeneo ya wateja wao.

Hazam anasema wameamua kuchukua jukumu la kumfuata mteja hadi kipimo kinakopelekwa, kumpa elimu namna gani arekebishe mwenyewe pale itakapotokea tatizo la kiufundi.

  Ushirikiano na Serikali

 Watoa huduma wa vipimo wamekuwa na ushiriakiano mzuri na serikali za awamu zote wakitoa huduma ya mizani katika taasisi za serikali na taasisi binafsi huku wakichukua jukumu la kutoa elimu ya matumizi kwa wateja na kuwaelimisha juu ya kuwa waaminifu hususani wale wanaotoa huduma kuhakikisha mteja hapunjwi kwa bidhaa inayohitaji kipimo cha mzani.

Anasema sambamba na hilo wauzaji wa vipimo wameboresha mazingira ya wateja wao wenye ulemavu wa viungo kwa kuagiza vipimo vinavyoendana na hali zao, mahali pa biashara, majira na nyakati.

 Anabainisha kuwa biashara ya mizani inahitaji uvumilivu, utu na kuthamini uhitaji wa mteja ndio maana sio bidhaa ya kupata kipato kikubwa ni huduma, ya kuwezesha wafanyabiashara wafanye  shuguli zao za biashara bila kupunjana uzito.

Ni huduma inayotakiwa kila mahali hata pembezoni mwa nchi na hivyo bali ni wito unaomsukuma muuzaji kutoa huduma sahihi na stahiki katika mazingira ya aina yoyote.

Sahel Tanzania wanasema dhana ya Tanzania ya viwanda inawezekana ikiwa kila mmoja wetu mwenye umri wa kufanya kazi akitimiza wajibu wake kwenye nafasi yake kwa wakati na zaidi ya yote kuwa na uzalendo wa kujituma na kuthamini chako.

Nyumbani kwanza ndio msisitizo wa watoa huduma wa vipimo (mizani ambao wamepania kuwa na viwanda vya kutengeneza mizani nchini Tanzania yenye viwango vya kimataifa.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles