30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Safu mpya CWT itatua kero za walimu

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimepata safu mpya ya uongozi, baada ya kufanya uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba yao.

Uongozi huo, utakuwa na kazi moja tu ya kuendelea mafanikio na mshikamano uliopo ndani ya walimu, badala ya kuwagawa kwa manufaa ya watu wachache wasiowatakia mema.

Tunasema hivi kwa sababu kumekuwapo na fukuto kwa muda ndani ya chama hiki, huku baadhi yao wakijaribu kutaka kuunda chama kingine, jambo ambalo halina tija hata kidogo kwa maendeleo  na uhai wake.

Tunakumbuka kabla ya uchaguzi huu, Rais Dk. John Magufuli alialikwa na kuwahutubia walimu kwa kirefu namna ambavyo Serikali imekuwa ikichukua hatua kuboresha utendaji kazi wao.

Rais alisema amejipanga kufanya mambo mazito kwa walimu, ikiwa ni pamoja na kulipa madeni yao yote kabla ya Agosti, mwaka huu, kuwapandisha madaraja na mambo mengine.

Wajumbe wa mkutano huo, wamechagua viongozi ambao wanaamini watasaidia kuwaongoza ndani ya miaka mitano ijayo.

Kwa mfano, wamemchagua,Deus Seif tena kuwa katibu mkuu kitendo ambacho kinaonyesha wana imani kubwa naye.

Seif anashika nafasi hiyo kwa mara ya pili mfululizo kwa kupata kura 491 kati ya kura 869 zilizopigwa. Hii ni dalili ya wazi ambayo inaonyesha namna ambavyo walimu wana imani kubwa naye.

Pia Leah Ulaya alitangazwa mshindi nafasi ya mwenyekiti kwa kupata kura 475, huku mpinzani wake akipata kura 365 kati ya kura 840 zilizopigwa.

Viongozi wengine,ni Makamu wa Rais, Dinah Mathaman ambaye alipata kura 428 na kumshinda aliyekuwa akitetea kiti hicho Christopher Banda ambaye alipata kura 375 kati ya kura 869 zilizopigwa .

Pia Naibu Katibu Mkuu, Maganga Japhet, huku  Alawi Abubakari akichaguliwa Mweka Hazina kwa kupata kura 534 kati ya kura 857.

Katika nafasi ya udhamini , aliochaguliwa ni Faustine Salala,Emmanuel Aloyce na Clement Mswanyama.

Wajumbe wa mkutano,Philipo Mahewa  mjumbe wa Tucta na  Evodius Heneriko akichaguliwa kuwakilisha kundi la walimu vijana.

Wajumbe  mkutano,walimchagua Shani Ulumbi kuwakilisha walemavu na Eliza Werema akiwakilisha wanawake.

Ni wazi safu hii, sasa lazima ijipange vizuri kama tulivyosema hapo juu kuwatumikia walimu.

Haiwezekani hata kidogo viongozi wachaguliwe imani kubwa kiasi hiki, lafu wanageuka wasaliti baada ya muda mrefu.

Kama tunavyotambua, walimu wana majukumu makubwa na wamebeba dhamana ya kuhakikisha taifa linakuwa na wasomo kuanzia ngazi ya chini hadi taifa.

Sasa ni wakati wa kuzaliwa upya na kuachana na mambo ambayo hayana tija kama ambavyo tumeshuhudia miaka ya hivi karibuni.

Tunategemea Ulaya na wasaidizi wake wana kazi kubwa ya kufanya, lakini wakitegemea zaidi kupata ushirikiano maana waswahili wanasema umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu.

Sisi  MTANZANIA, tunaamini sekta hii ni muhimu na ndiyo imekuwa ikizalisha wataalamu katika sekta zingine.

Kwa kuwa serikali imeahidi kushirikiana nayo kwa kila hatua, sasa walimu wakazi moja tu ya kuhakikisha hawaangushi mwajiri wao.

Siku zote tunatambua kuna changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo kila siku kwenye utendaji wao, jambo kubwa mwajiri amesema atawasaidia, hivyo lazima nao waonyeshe wako tayari.

Serikali na walimu ni ni kitu kimoja, wote wanajenga nyumba moja, hivyo basi kila upande unapaswa kutimiza wajibu wake.

Tunamazia kwa kusema safu mpya CWT itatue kero za walimu, epukeni migogoro isiyokuwa na tija.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles