24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Safari za Treni ya SGR kuanza Julai

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Serikali imesema kuwa Safari za treni ya umeme(SGR) kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro zinatarajiwa kuanza Julai, mwaka huu ambapo hadi sasa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa umekamilika kw asilimia 98.

Hayo yamebainishwa leo Juni 9, 2023 na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete wakati wa hafla ya kupokea mabehewa sita ya ghorofa kati ya 30 yaliyoagizwa nchini Ujerumani kwa ajili ya abiria.

Amesema mabehewa hayo yalifanyiwa maboresho na Kampuni ya Luetkemeyer Transport and Logistic (GMBH) yaliwasili nchini Jumanne wiki hii.

“Safari za treni ya umeme zitaanza pindi vichwa vya treni viwili vitakapowasili nchini Julai, mwaka huu na kuanza safari za mikoa miwili Dar es Salaam na Morogoro na leo tumepokea mabehewa sita ambayo ni ya gorofa na baadae kuendelea na mikoa mingine,” amesema Mwakibete.

Amesema daraja la pili la mabehewa hayo litabeba abiria 123 na daraja la tatu abiria 140 na wizara kupitia TRC itaendelea kusimamia ununuzi vitendea kazi kuhakikisha kwamba vinafika kwa wakati.

Amesema mikataba iliyosainiwa ni mabehewa 59 kutoka Korea, mabehewa ya mzigo 1,430 kutoka China na vichwa vya treni EMU seti 10.

Amesema kuwepo kwa safari za treni ya umeme kilometa 160 kwa kasi saa moja zitarahisisha shughuli za kibinadamu za kiuchumi maendeleo na kusafiri kwa haraka kuokoa muda.

Amesema nchini zaidi tano zimeonyesha utayari wa kujenga reli ya kisasa kiwango cha kimataifa (SGR) kupitia ubia katika ushoroba wa Mtwara ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alimshukuru Rais Dk. Samia Suluhu kwa kusimamia shirika hilo na kutoa takribani
Sh trilioni 23 kwa miradi ya ujenzi wa reli.

“Mabehewa hayo ni ya kisasa na yamegharimu euro milioni 26.6 huku behewa moja la gorofa ni sawa na abiria wa mabasi matatu na kitakachofuata sasa ni kichwa cha treni ambacho kinatarajia kufika Julai mwishoni kianze kufanya kazi mwaka huu,”amesema Kdogosa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles