24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 23, 2023

Contact us: [email protected]

Safari ya Samatta Ubelgiji yaiva

samattaNA SAADA SALIM, DAR ES SALAAM

MMILIKI wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Moise Katumbi, amekubali yaishe na kuamua kumruhusu Mbwana Samatta kujiunga na timu ya K.R.C Genk ya Ubelgiji, baada ya straika huyo kuzidi kupiganiwa barani Ulaya.

Samatta na bosi wake wamekuwa wakivutana kwa muda wa wiki tatu sasa, ambapo Samatta alitaka kwenda kucheza soka Ubelgiji wakati mmiliki huyo akiwa na mpango wa kumuongezea mkataba ili aweze kumuuza kwa klabu ya Nantes ya Ufaransa.

Straika huyo ambaye alipata tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, tayari amesaini mkataba wa awali wa miaka minne na klabu ya Genk na alitarajiwa kurejea nchini jana usiku kutoka Kongo kwa ajili ya kwenda kukamilisha taratibu.

Meneja wa mshambuliaji huyo, Jamali Kisongo, alilithibitishia MTANZANIA jana kuwa kila kitu kilikwenda sawa baada ya Katumbi kumkubalia Samatta kujiunga na timu anayopenda kucheza.

Samatta na Genk wanafanya mpango wa kukimbizana na muda ili kuwahi usajili wa dirisha kabla haujafungwa, ili mwezi ujao nyota huyo aanze kukipiga katika michuano ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.

“Ikumbukwe kuwa Samatta alisafiri kwenda Lubumbashi kwa mambo mawili muhimu, kuruhusiwa kuichezea Genk au kuendelea na mkataba wake TP Mazembe ili ukimalizika mwezi Aprili aondoke kama mchezaji huru,” alisema Kisongo.

Alisema Samatta aliondoka jijini Dar es Salaam Januari 20, mwaka huu kuelekea DRC akiwa ameambata na Ofisa mmoja wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwa ajili ya kwenda kumshawishi bosi wa TP Mazembe akubali kumruhusu kujiunga na Genk badala ya Nantes ya Ufaransa.

Nantes ilikuwa tayari kulipa dau la Euro milioni moja (zaidi ya Sh bilioni 2.3 za Kitanzania), ili kumnasa Samatta, ambapo TP Mazembe ingenufaika na mgawo wa asilimia 25 kama mshambuliaji huyo angeuzwa kwa klabu nyingine.

Klabu ya Genk ipo tayari kutoa kiasi cha Euro 800,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.8 za Kitanzania) kumnunua Samatta na imekubali kuipa TP Mazembe mgawo wa asilimia 20 kama straika huyo atauzwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles