Mnamo tarehe 1 Julai 2017, shirika la ndege la Precision Air limezindua safari kati ya
Tanzania na Uganda na kuwapa nafasi wananchi wa nchi zote mbili kunufaika na
safari hizo kati ya Dar es Salaam-Kilimanjaro – Entebbe kwa kuongeza ufanisi katika
shughuli zao.
Nilibahatika kuwa mmoja ya abiria katika safari ya uzinduzi wa safari hizo, safari
ilianzia katika uwanja wa Julius Nyerere majira ya saa 1:10 Asubuhi,ambapo
nilijumuika na wasafiri wengine waliokuwa wakisubiri kwa shauku kubwa kuanza safari
huku wakiwa tayari na pasi zao za kusafiria pamoja na tiketi zao.
Abiria wote tulifanya utaratibu wakugonga hati zetu za safari kwa maofisa wa idara ya
uhamiaji na kuelekea katika eneo la kusubiri kuitwa kwa ajili ya kupanda ndege na
kuianza safari. Ilikua ni asubuhi nzuri, hali ya hewa ilikua ya kaubaridi huku jua
likichomoza kwa mbali. Zikisikika sauti za ngurumo za ndege zilizokuwa zikiondoka
uwanjani hapo na matangazo mabali mbali uwanjan hapo. Baada ya dakika kadhaa
nikiwa nimesimama karibu na geti namba tano nikiendelea kufurahia mandhari ya
uwanja wetu wa ndege, ilisikika sauti iliyojaa bashasha ya ukarimu ya muongoza
ratiba ya usafiri akitoa tangazo kwa abiria wote waliokuwa wakielekea Uganda
kufuata utaratibu wa kuanza kuhakiki pasi zao iliwaingie kwenye ndege tayari kuianza
safari.
Sio siri, huduma zilikuwa za kiwango cha juu kuanzia mapokezi ya abiria walipowasili
uwanjani hadi kwenye zoezi zima la kuhakiki pasi.
Mlangoni kwenye ndege alikuwa amesimama mwanadada mrembo, aliyekua amevalia
nadhifu kwenye sare za Precision Air, Huyu ni Halima Njau aliyekuwa mmoja wa
wahudumu wa Precision Air waliokuwa wenyeji wetu kwa kipindi chote cha safari
kuelekea Enteebe. Aliwakaribisha abiria wote kwa ukarimu na tabasamu la upendo
huku muhudumu mwingine wakiwapokea abiria na kuwaonyesha kila mmoja nafasi
yake.
Baada ya dakika kadhaa Rubani na muhudumu waliwaandaa abiria wote kwa tangazo
kuhakikisha kila kitu kiko sawa, na hatimaye ndege ilianza safari.
Baada ya takribani lisaa limoja ndege ilitua uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, KIA
ambapo ndege ilikaa hapo kwa muda dakika 20 kwa ajili ya kuruhusu abiria waliokuwa
wakiishia Kilimanjaro kuteremka na kupakia wale waliokua wakienda Entebbe kutoke
a Kilimanjaro na Arusha kupanda. Wakati tukiwa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro
niliweza kushuhudia ni jinsi gani Precision Air inautumia vyema uwanja wa
Kilimanjaro. Nilishuhudia ndege mbili zikitua katika uwanja huo, ndipo nilipo patwa
na shauku ya kutaka kujua safari za Precion Air kutoka katika uwanja huo. Baada ya
kudodosa nilielezwa ya kuwa kutokea Kilimanjaro Precision Air inasafari za kwenda
Mwanza,Zanzibar,Dar es Salaam, Nairobi na sasa Entebbe. Hili lilinifanya kutambua
mchango muhimu unaotolewa na shirika la Precision Air katika huduma ya usafari wa
anga hapa nchini.
Baada ya dakika 20 za mapumziko, tuliendelea na safari kuelekea Entebbe.
Waaoow…!! Ndivyo nilivyomskia abiria mmoja akifurahia kuuona mlima Kilimanjaro
muda mfupi baada ya ndege kuruka, Rubani alitueleza tulikua tukikatiza katikati ya
Mlima Kilimanjaro, uliokua upande wa kulia na Mlima Meru uliokua upande wa
kushoto. Niliwaona baadhi ya abiria hasa wakigeni wakifanya juhudi za kupata picha
za vivutio hivyo na hali hiyo ilinifanya nijisikie fahari kua Mtanzania. Haikuchukua
muda mrefu ambapo kabla ya Rubani hajatutaarifu tena kuwa tulikua tukikatiza kando
ya Mlima Oldanyengai ambao una volcano hai, tuliweza kushuhudia michirizi ya majivu
ikiupamba mlima huo katika kilele chake, ushahidi tosha kua volcano yake ii hai na
inatokota.
‘ona nikama mlima ule unafuka moshi…..’ alisikika mmoja wa abiria akimueleza
mwenzake. Hakika Ilikiua dhahiri ya kua kila abiria alifurahia alichokua akikiiona, na
kwa mda nilijikuta nikitamani kuwa mmoja wa wasafiri wa kila mara kuelekea
Entebbe.
Kilichotia fora zaidi katika safari nzima, ni rubani wa ndege hiyo kwa jina la Manasse
alipotuarifu abiria wote kutazama chini ili kuufurahia muonekano wa kuvutia uliokuwa
ukionekana kutoka juu.
Kwa mara ya kwanza, binafsi niliweza kuuona mlima Oldonyo Lengai kwa muonekano
kutoka angani,na kilichonifurahisha zaidi ni rubani kuahakikisha anapita katika usawa
sahihi ili abiria waweze kupata muonekano mzuri zaidi.
Safari yetu ilikua murua kabisa, na mara zote jirani yangu alikua akinileza ni jinsi gani
alikua akifurahia safari ile huku akiusifia utulivu wa ndege angani uliomfanya asinzie
mara kwa mara.
Baada ya masaa mwendo kidogo rubani alituhabarisha tena yakuwa tulikuwa tukipaa
juu ya ziwa Victoria, tuliweza kushuhudia ukubwa wa ziwa Victoria kutoka angani, na
kadri tulivyokuwa tukikaribia Entebbe tulianza kuona visiwa vichahce ziwani, na kwa
mbaali tuliweza kuona mitumbwi ya wavuvi. Hakika ilikua safari ya kipekee.
Tulipowasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe, ndege ilitua salama. Tayari
kumbukumbu ya safari ilikua ikijirudia kichwani mwangu, picha za mandhari nzuri
nilizo ziona toka mwanzo wa safari zilikua zikijirudia kichwani mwangu. Matone ya
maji kwenye dirisha yana nirudisha kwenye wakati halisi, hii haikua mvua bali ni
salamau maalumu ya kutukaribisha rasmi katika uwanja wa ndege wa Entebbe, salamu
hii hutolewa kwamagari mawili ya zima moto kurusha maji hewani huku yakitazamana
na ndege hukatiza katikati. Ishara hii ili ashiria kuanza rasmi kwa safari za Precision
Air nchini Uganda.
Wahudumu pamoja na rubani walitutakia abiria wote kheri kabla ya kushukuru na
tiliposhuka chini tulikaribishwa na wahudumu wengine wa Precision Air kwa furaha.
Safari hili kwangu binafsi imekuwa ya aina yake kupaa na Precision Air, na sita sita
kumshawishi mtu yeyote kusafiri na Precision Air, kwani nna uhakika hata yeye
ataifurahia.
Nikiwa naandika haya yote, naendelea kutafakari ni jinsi gani Tnazania na Uganda
watanufaika na safari hizi za Precision Air. Tayari nawaona wafanyakazi wa Jumuiya
yetu ya Afrika mashariki wakitumia safari hizi katika kuongeza ufanisi katika utendaji
wao kwa zile shughuli zinazo wahitaji kusafiri. Nawaona pia wafanyakazi wa mradi wa
bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga nchini Tanzania wakiitumia Precision Air
katika kufanikisha shughuli zao za kiutendaji. Wakati huo huo nawaona wananchi wa
Uganda wakitumia fursa ya safari hizi kufanya utalii kwa vivutio kama Zanzibar na
Serengeti.
Nawaona pia wafanyabiashara wa mavazi na urembo kutoka Tanzania
wanavyochangamkia safari hizi katika kuongeza tija katika biashara zao.
Binafsi niseme asanteni Precision Air kwa fursa hii, kwani kupitia mtandao wenu wa
safari zenu mmeendelea kuifungua Tanzania. Naisubiri kwa hamu ile siku ntapata
fursa ya kusafiri na nyinyi tena.