27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

SADC yaridhishwa na demokrasia, utawala bora Tanzania

Na Mwandishi wetu-Lusaka

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dk Stagomena Tax, amesema Tanzania imepewa nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo kutokana na kutimiza vigezo vinavyohitajika na ambavyo ni uwepo wa demokrasia na utawala bora.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Tax alisema hayo baada ya kumalizika mkutano wa 21 wa kamati ya mawaziri kuhusu asasi ya siasa, ulinzi na usalama ya SADC  kinachofanyika Lusaka Zambia.

Taarifa hiyo ilisema Dk Tax, alizitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuendelea kukuza demokrasia na utawala bora kwa kuwa ndio nguzo muhimu za jumuiya hiyo.

“Licha ya uchanga wa demokrasia katika ukanda huu, nchi zimeendelea kupiga hatua katika kuboresha demokrasia na utawala bora na Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazozingatia uwepo wa demokrasia na utawala bora miongoni mwa nchi wanachama,” taarifa ilimnukuu Dk Tax.

Ilisema pia mkutano huo umeridhishwa na ukuaji wa demokrasia na utawala bora miongoni mwa nchi wanachama kutokana na chaguzi zilizofanyika kwa haki, uhuru na amani katika nchi takribani sita ikiwemo Afrika ya Kusini, Eswatini, Malawi, Madagascar na Congo DRC.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, alisema kumalizika kwa chaguzi katika nchi sita wanachama wa jumuiya hiyo, kunaidhihirishia dunia namna ambavyo Ukanda wa Kusini mwa Afrika ukiyasimamia mambo yake yenyewe bila ya kuingiliwa na mataifa mengine una uwezo wa kuimarisha taasisi zake za demokrasia, utawala bora na haki jambo ambalo Tanzania.

Alisema mkutano huo pia umejadili maombi ya Burundi kujiunga na jumuiya hiyo ambayo yamekuwepo kwa takribani miaka mitatu sasa, na kutanabaisha kuwa Burundi imetekeleza kwa kiwango cha asilimia sabini masharti iliyotakiwa kuyatimiza ili kupata ridhaa ya kuwa mwanachama wa SADC .

Alisema asilimia 30 yaliyosalia, Tanzania kwa kushirikiana na sekretarieti ya SADC  na nchi nyingine wanachama zitaendelea kuisaidia Burundi ili iweze kuwa mwanachama jambo litakaloisaidia Burundi kuimarika kisiasa na kidemokrasia na kushiriki katika maendeleo ya Bara la Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles