DRC, Kongo
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mwenzake wa Botswana, Eric Mokgweetsi Masisi wamekubali kuendelea kuzungumza kutafuta suluhisho kuhusu suala la wadhifa wa Katibu Mtendaji wa SADC.
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mwenzake wa Botswana Eric Mokgweetsi Masisi wamekubali kuendelea kuzungumza kutafuta suluhisho kuhusu suala la wadhifa wa Katibu Mtendaji wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika-SADC.
Akiwa ziarani mjini Kinshasa jana Jumatatu, Rais Masisi alizungumza ana kwa ana na Tshisekedi. Viongozi hao wawili wamejadili maswala mengine kadhaa yakiwemo na kupambana na janga la Covid-19.
Botswana ilikuwa ya kwanza kuwasilisha ombi la kugombea nafasi ya Katibu mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC. Nafasi hiyo itakuwa wazi Agosti ijayo, lakini hii imekutana na changamoto baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia kutangaza pendekezo lake.