31.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

Sababu zitakazoifanya Simba kuendelea kutamba

 ZAINAB IDDY 

SIMBA ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzanai Bara kwa misimu mitatu mfululizo sasa, lakini pia ni washindi wa Kombe la Shirikisho, maarufu Kombe la Azam. 

Zaidi ya hayo, Simba ni washindi wa Ngao ya Jamii,kwa miaka minne mfululizo, hii ni rekodi tamu. 

Hakuna ubishi kwa misimu mitatu , kutokea msimu huu hasa baada ya Azam FC kuonekana angalau wanarudi katika ushindani ule wa misimu mitano iliyopita. 

Katika kipindi hiki cha miaka mitatu Simba wakichukua mataji ya mashindano mbalimbali mfululizo yapo maeneo muhimu ambayo kama timu nyingine zitaweza kuyamudu bila shaka taji litaondoka mikononi mwao. 

UPANA WA KIKOSI 

Achana na nyota 11 wanaoanza pale Simba, benchi lao nalo ni tamu kuna wachezaji mahiri pia. 

Katika mechi za mwanzo za ligi Meddie Kagere, Chris Mugalu, Hassan Dilunga, Fransis Kahata,Ibrahim Ajib na wengineo waliobnekana kuanzia benchi. 

Kukaa kwao benchi haina maana viwango vimeshuka kwani mara baada ya kutakiwa kuanza au kuingikia wameonekana kuwa bora zaidi ya vikosi vya timu nyingine vinavyotegemewa kuanza. 

MFUMO WA UONGOZI 

Katika hili hakuna ubishi kuwa, kwa sasa Simba ina mfumo wa uongozi unaoeleweka huku wengi wao wakiwa na uzoefu mkubwa na soka la Tanzania. 

Simba ipo chini ya Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez halafu juu yake ipo Bodi ya Wakurugenzi ambayo hukutana mara kwa mara kulingana na uhitaji wake. 

Hili ni tofauti na klabu kama Yanga, Azam au timu nyingine za ligi kuu mfano kwa watani wao Yanga viongozi waliopo hawana uzoefu huku mfumo wa uongozi ukiwa bado si rafiki kuingia katika soka la ushindani la la kibiashara. 

MASLAHI MAZURI 

Msimu huu Yanga chini ya wadhamini wao Kampuni ya GSM imetumia fedha nyingi kufanya usajili kuliko Simba. 

Hata hivyo, bado ukweli unabakia kuwa Wekundu wa Msimbazi ndio klabu inayolipa nyota wake maslahi mazuri kuliko timu nyingine zilizosalia katika Ligi Kuu Tanzania Bara. 

Kwa mujibu wa Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji’Mo’, bajeti ya mishahara ya klabu hiyo kwa mwezi inafikia Sh. Milioni 250. 

Uchunguzi wa SPOTIKIKI, umebaini bajeti ya mishahara kwa Yanga haifiki Sh milioni 180. 

UWANJA WA MAZOEZI 

Wakati Yanga ikiwa inapambana kuanza ujenzi wa uwanja wake huko Kigamboni jijini Dar es Sa laam, Simba tayari inamiliki viwanja viwili vya mazoezi eneo la Bunju. 

Viwanja hivi vya mazoezi vya Simba, kimoja kimetandikwa nyasi bandia na kingine kina nyasi za asili. 

Hatua hii ya Simba kumiliki viwanja vyake vya mazoezi, si tu kimeipungumzia klabu hiyo gharama ya kukodi viwanja,pia kinaipa nafasi timu hiyo kufanya mazoezi kwenye eneo zuri la kuchezea. Hili linasaidia maelekezo ya makocha kufanyiwa kazi kwa ufanisi na wachezaji. 

Tumekuwa tukishuhudia kwa jinsi falsafa ya Simba ambayo ni kucheza soka la pasi fupi fupi inavyokubali wakati huu. 

Hii ni kutokana na wachezaji kufanya mazoezi kwenye eneo zuri la kuchezea. 

Hata hivyo bado Simba inahitaji kuviendeleza zaidi ili viweze kutumika kwa baadhi ya michezo yake ya Ligi Kuu hapo baadaye. 

USHIRIKI KIMATAIFA 

Kwa mara nyingine Simba itaiwakilisha Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Namungo itapeperusha bendera ya nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. 

Ushiriki wa michuano ya kimataifa kwa miaka minne mfululizo ni jambo ambalo Simba imewazidi wapinzani wao wa karibu Yanga wakati huu. 

Fursa hii imewafanya viongozi wa Simba chini ya mwekezaji Mo, pia kuwa na mipango thabiti ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika ,ligi lakini pia katika michuano ya kimataifa. 

Na zaidi, uongozi wa klabu hiyo unataka kufikia kuvunja rekodi ya klabu hiyo ya kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo umekuwa ukiweka mikakati mikubwa ya kuhakikisha hilo linafanikiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,507FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles