25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SABABU YA SANCHEZ KUSHINDWA KUONDOKA ARSENAL

LONDON, England

JUHUDI za klabu ya Manchester City kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez ziligonga mwamba siku ya mwisho, baada kukosekana mchezaji wa kujaza nafasi yake.

Inadaiwa kwamba, Manchester City na Arsenal walifikia makubaliano, kwa masharti kuhusu kuhama kwa Sanchez (28).

Ada ya uhamisho wake ilikuwa pauni milioni 55, na ziada ya pauni milioni 5 ambapo inafanya jumla kuwa pauni milioni 60, lakini ilitegemea kufanikiwa kwa Arsenal kumpata mchezaji wa kujaza nafasi yake.

Mchezaji waliyemtaka zaidi alikuwa winga wa Monaco, Thomas Lemar, ambaye inadaiwa alikataa kuhamia Arsenal.

Monaco walikuwa wamekubaliana na Arsenal kuhusu uhamisho wa Lemar (21) kwa pauni milioni 90.

Endapo Sanchez angejiunga na Manchester City, angeunganishwa tena na kocha wake wa zamani, wakati akicheza Barcelona, Pep Guardiola.

Mchezaji huyo wa Chile anatumikia mkataba wake wa mwisho Emirates na kuna uwezekano mkubwa kwamba ataondoka majira yajayo ya joto akiwa huru.

Mchezaji aliyendoka Arsenal siku ya mwisho ni mshambuliaji Lucas Perez, ambaye alijiunga na timu hiyo msimu uliopita kwa pauni milioni 17.

Perez alirejea klabu yake ya awali, Deportivo La Coruna, kwa mkopo baada ya kufunga mabao saba katika mechi 21 alizowachezea Arsenal.

Sanchez alichezea Arsenal mara ya kwanza msimu huu Jumapili iliyopita katika mechi waliyolazwa mabao 4-0 na Liverpool.

Sanchez alijiunga na Arsenal kutoka Barcelona mwaka 2014 kwa ada ya takriban pauni milioni 35 na alishinda kombe lake la pili la FA akiwa na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita.

Mapema mwezi huu, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, alisema Sanchez ataheshimu uamuzi wake wa kutaka kusalia naye mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles