23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SABABU WAKE WA WATU KUCHEPUKA NA WANAUME WANAOFANYA MAZOEZI

Na LEONARD MANG’OHA,

MAZOEZI ya viungo yanaelezwa kuwa nguzo na kinga kuu dhidi ya magonjwa mbalimbali hususan yasiyo ya kuambukiza. Pia huuweka mwili katika hali nzuri na kumfanya mtu kuwa shupavu.

Kutokana na hali hiyo, jamii imekuwa ikisisitizwa kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa ya sukari, saratani na shinikizo la damu ambayo husababishwa na mambo mbalimbali ikiwamo ulaji ovyo usiozingatia kanuni za afya ukiambatana na kutofanya mazoezi.

Katika chapisho moja lililochapishwa katika blogu ya Jamii Active na Mtaalamu wa Fiziolojia ya Mazoezi na Homoni katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Dk. Fredrick Mashili, linaeleza kuwa mazoezi husababisha kasi ya mapigo ya moyo na ile ya kupumua kuongezeka.

Dk. Mashili anasema mazoezi hayo yanahusisha vitendo kama kutembea, kukimbia kwa mwendo wa kawaida, kuruka kamba na kucheza muziki ambayo kitaalamu huitwa ‘aerobics’ au `cardio´.

Anasema mazoezi haya hutegemea zaidi kasi inayotumika wakati wa kufanya mazoezi na hutumia hewa ya oxygen kwa kiasi kikubwa.

Anaeleza kuwa mazoezi haya huimarisha afya ya moyo na mapafu hivyo kuupa mwili uwezo wa kufanya kazi bila kuchoka mapema (endurance) na husaidia kujikinga na maradhi sugu yasiyoambukiza kama vile kisukari na magonjwa ya moyo.

Hivi majuzi MTANZANIA lilipata taarifa kuwa kumekuwa na tabia ya wanawake wengi waliolewa na wanaume ambao hutumia muda mwingi kutafuta fedha, hupenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na vijana wanaofanya mazeozi.

Sababu kubwa ya wanawake hao kupenda kuchepuka na wanaume wafanya mazoezi, inatajwa kuwa ni kutoridhishwa na waume zao ambao wako bize na kazi hivyo hawana muda.

Inasemekana kuwa wanaume wengi wanaofanya kazi hawapati muda wa kufanya mazoezi kutokana na uchovu unaotokana na majukumu ya kila siku ambao husababisha kushindwa kushiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu kiasi cha kuwaridhisha wenzi wao.

Hivyo, wanawake wengi walioolewa hulazimika kwenda sehemu za kufanyia mazoezi (gym) ili kufanya mazoezi na wakiwa huko huanzisha uhusiano na vijana wakakamavu ambao huwapa kile wanachokihitaji.

Katika baadhi ya gym ambazo MTANZANIA ilizunguka kufanya utafiti, ilibaini kuwa hali hiyo imeshamiri zaidi kwa wanawake hao ambao hufanya kila namna kuhakikisha wanatoka na vijana.

Akizungumzia suala hilo, msimamizi wa mazoezi  (Gym Master) katika gym iliyopo Hoteli ya City Style, Saleh Kambi anasema suala la wanawake kupenda wanaume wanaofanya mazoezi lipo na kwamba ameshuhudia vitendo hivyo vikifanyika mara kwa mara.

Anasema kuwa si katika gym aliyopo sasa tu bali sehemu nyingi za mazoezi wanawake tena ambao wanaonekana wana ndoa zao huwa wanajihusisha mapenzi na vijana wakakamavu.

Anasema hii huenda ni kwa sababu mazoezi husaidia kumudu tendo la ndoa kwa muda mrefu akitolea mfano watu wanaocheza mpira wa miguu kuwa ni watu wenye uwezo mkubwa wa kumudu tendo hilo kwa sababu huwa wanyumbulifu (flexibility) kutokana na aina ya mazoezi wanayofanya kuhusisha maeneo yote ya mwili.

“Unajua kwa kawaida mazoezi huongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Mtu asiyefanya mazoezi ili amridhishe mwanamke lazima anywe pombe au atumie dawa za kuongeza kuvu.

“Tabia ya kina dada kupenda  wanaume wanaofanya mazoezi ipo sana, ila sijafahamu ni kwanini. Ninachofahamu ni kwamba unapokuwa na mazoezi kwa kawaida lazima utawavutia wanawake kutokana na mwonekano wako.

Ukiwa na kitambi mwanamke atakuwa na wewe kwa sababu ya fedha zako mambo mengine atayatafuta kwa vijana wanaofanya mazoezi,” anasema Kambi.

Naye Stanley Timoth, mfanyakazi katika mgodi wa Geita (GGM) anasema suala hilo halipo kwa wanawake walioolewa pekee bali hata kwa wasioolewa, huku baadhi yao wakiwachukulia wanaoume wenye mvuto wa kimazoezi kuwa walinzi wao dhidi ya maadui.

Anasema wanawake wengi hupenda kumwona mwanamume shupavu na mwenye mwili uliojengeka na si legelege wakiamini kuwa mwanamume anayefanya mazoezi huwa na nguvu na pumzi ya kumudu tendo la ndoa kwa muda mrefu – hachoki haraka.

“Wanataka mwanamume anayewaridhisha na kupata kile wanachokihitaji katika tendo hilo,  kama umezoea kufanya mazoezi ukiacha ni lazima utaona mabadiliko hata kutoka kwa mwenzi wako,” anasema Timoth.

Janeth Fratern (25) anayefanya shughuli za ujasiriamali anasema kwake mazoezi ni kitu cha lazima na hufanya hivyo kuhakikisha anakuwa salama kiafya na kuepuka magonjwa.

Anasema huwa anapendelea kufanya mazoezi katika eneo la wazi bila kutumia mashine ila huzitumia pale tu inapomlazimu.

Anasema mazoezi humsaidia kuwa na nguvu na ajiamini, pia humwondolea ‘nyama uzembe’ hivyo kuwa na umbo analolihitaji.

Anaeleza kuwa wanaume wanaofanya mazoezi huwa na mvuto wa kimaumbile na nguvu wakati wa tendo la ndoa.

“Mwanamume asiyefanya mazoezi ni mara chache kukufikisha kileleni, anatumia muda mfupi kuliko anayefanya mazoezi, huwezi kufurahia tendo la namna hiyo kama si mvumilivu ni lazima utachepuka ili kutafuta mwanamume atakayeweza kukidhi mahitaji yako.

“Kuna tofauti kubwa unaposhiriki tendo la ndoa na mtu anayefanya mazoezi na Yule asiyefanya. Mtu anayefanya mazoezi huwa ni mwepesi katika mambo mbalimbali hauwezi kupoteza hamu ya kuwa naye,” anasema Fratern.

Anasema amekuwa akionekana msichana wa kipekee katika jamii, na anafurahishwa kuona jamii inaanza kuzoea utaratibu wa kufanya mazoezi kwa jinsia zote.

“Nawashauri rafiki zangu na wasichana wengine kufanya mazoezi, kwani baadhi yao wanalazimika kutafuta usafiri hata eneo la kutembea kwa dakika kumi tu kwa kuhofia kuchoka,” anasema Fratern.

Alex Uronu ni mtaalamu wa masuala ya habari na teknolojia na mmoja wa vijana wanaofanya mazoezi kila siku, anasema hufanya mazoezi ili kuimarisha  afya yake na kuepuka uzito mkubwa.

Kuhusu suala la wanawake walioolewa na watu wazima wasiofanya mazoezi kuwa na uhusiano na vijana wanaofanya mazoezi, anasema amekuwa akilisikia suala hilo mara nyingi tena kwa wanawake wenyewe.

Anasema wanawake wengi wanaeleza sababu ya kufanya hivyo kuwa ni kupata ulinzi, kwamba wanaamini kuwa wanapokuwa na mtu anayefanya mazoezi wanakuwa katika hali ya usalama dhidi ya dhuluma na uonevu katika jamii, pia kuridhishwa kimapenzi.

Anasema wanawake wengi hawapendi wanaume wazembe na magoigoi.

“Wanawake hupenda wanaume wenye uwezo wa kutatua matatizo yao, hasa yale yanayohitaji kutumia nguvu, ukiwa legelege wanakudharau.

“Wengine wanaamini mwanamume anayefanya mazoezi si tu anakuwa vizuri kimwili hata kiakili anakuwa vizuri zaidi ya mtu asiyefanya mazoezi,” anasema Uronu.

Kwa upande wake Stanslaus Kawawa (50) anasema hana uhakika kama suala la mazoezi linaweza kusambaratisha ndoa.

Hata hivyo, anasema wengi wamekuwa na mwamko mkubwa wa kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa.

Dk. Mashili anasema tendo la ndoa kiuhalisia huhitaji nguvu hivyo inawezekana hiyo ikawa ni moja ya sababu zinazowafanya wanawake kuingia katika uhusiano na vijana.

Anasema kisayansi kadiri umri unavyokwenda uwezo na nguvu hupungua hivyo ni wazi kuwa hata uwezo wake katika tendo hilo hushuka siku hadi siku.

“Mazoezi ya viungo yanasaidia japo wengi hawaamini katika hilo, linapokuja suala la wanawake kupenda kuwa na uhusiano na watu wanaofanya mazoezi, wengi wanahusisha na mwonekano lakini naamini ni zaidi ya hapo.

“Kwa sababu hawa vijana nao wanakuwa katika uhusiano hivyo wanafahamu fika wanawake wanahitaji nini kutoka kwao. “Kwa kawaida wanawake hawana tabia ya kusema kama unakuwa umefanya vibaya ila kwa mtu aliyefanya vizuri watamwambia, naamini hao vijana wao wanaambiwa,” anasema Dk. Mashili.

Anaeleza kuwa tendo hilo hutegemea zaidi mzunguko wa damu katika mwili, hivyo kwa watu wanaofanya mazoezi ya mpira wanakuwa katika nafasi nzuri wanapokuwa katika tendo la ndoa.

Anasema wachezaji wa mpira huwa katika nafasi nzuri kutokana na aina ya mazoezi wanayofanya yanayohusisha kukimbia, hali inayoufanya mfumo wa damu kuwa mzuri kati ya sehemu moja na nyingine mwilini.

Dk. Jennifer Landa kupitia mtandao wa Fox News Health anaeleza kuwa kuna uhusiano wa wazi na uliothibitishwa kati ya mazoezi na tendo la ndoa. Anasema unapofanya mazoezi ubongo huzalisha ‘endorphins’ inayozalisha homoni za uzazi.

Anasema homoni hizi hupunguza mapigo ya moyo, huboresha mmeng’enyo na hupunguza shinikizo la damu hivyo kuufanya mwili kuwa katika hali nzuri.

“Mazoezi huweza kukufanya kuwa na ari ya tendo la ndoa, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa stamina na mshindo bora,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles